Hata wana magamba wanawakubali wabunge wa chadema

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
jamani tuwe wakweli, kwa wanaofuatilia bunge wanakubali kuwa wabunge wa chadema ndio watetezi wakubwa wa watanzania. sio kwamba watz hawaoni kuwa tatizo lao ni namba tu. kuna mwanamagamba ninae hapa ameamua kujiunga chadema kwa maelezo kwamba kikubwa unahitaji maslahi yako yatetewe na kama magamba hawawakilishi maslahi yake kwanini aendelee kuwaunga mkono? nawauliza magamba, una uhakika maslahi yako yanatetewa na magamba?
 
Nape aliwalaghai wa tz na porojo zake,sasa siku 90 zimekwisha na magamba bado hayavuka....Nape anapiga makelele mtaani bungeni magamba yanatetewa kwa nguvu zote. Alianza Lowassa kwa kushangiliwa eti serikali inaogopa kufanya maamuzi magumu...akaonekana shuja leo ilikuwa zamu ya gamba no.2 chenge tutarajie gamba no.3 LA atakavyo tetewa bungeni.... Habari ya kujivua gamba itabaki nadharia na ndoto za Nape na boss wake Mkama!
 
ccm wanatetea ruling class ambayo idadi yao haizidi asilimia moja. chadema wanawatetea wananchi ambao ni asilimia 99. wewe upo kundi gani? ukiwatetea ccm wakati haupo kwenye ruling class utakuwa umetumika tu sawa na mtu anayeshika pembe wanaokamua na kunywa maziwa ni wengine
 
Back
Top Bottom