Hata wana CCM tunashituka: Katiba ya kuwapa viongozi immunity!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,290
24,114
Ni wazi sasa hivi kwamba Katiba imekuwa ikifanyiwa maraekebisho ya mara kwa mara, kwa convenience ya watu na siyo manufaa ya moja kwa moja ya nchi.

Serikali ilipitisha miswaada na kupitisha Bungeni merekebisho ya Katiba hivi karibuni ili viongozi wa juu kabisa akiwemo Rais, Makamu wa Rais, Spika, Makamu wa Spika Mwanasheria Mkuu.

Hapa dhana ya uwajibikaji katika madaraka inapotea.

Sasa sisi wananchi tunapodai uwajibikaji kikatiba, kama mmoja wa waliopo juu watafanya jambo kinyume na sheria, haki itapatikana wapi?

Hii Katiba tuliyonayo tukiendelea kuisuka suka kuwa kwa convenience ya watawala, hilo si jema kwa mustakabali wa nchi.

Na hili tunalisema hata sisi wana CCM maana tuliyoyaona Awamu ya Tano yanatosha.

Katiba iwe kwa manufaa ya wananchi, si watawala.
 
... March 17, 2021 was the greatest milestone of this nation. Ni tarehe ambayo, sio kwamba umuhimu wake ni tukio lenyewe, bali ni mwanzo wa fikra na mtazamo mpya kama taifa. Ni tarehe ambayo inatukumbusha matokeo ya maamuzi yetu kwa umoja wetu; tunafikiri sawa sawa kabla ya kuamua? Au tunaamua tu kwa ushabiki wa kimakundi na msukumo wa maslahi binafsi bila kuzingatia athari za maamuzi yetu hayo kwa nchi na vizazi vijavyo?

Nyenzo zetu (Katiba, sheria, mifumo, n.k.) iko stable kutusaidia pindi tukikosea kimaamuzi au tuliyemwamini akatutenda ndivyo sivyo? Au tunaamua kukabidhi mamlaka na madaraka yetu kwa wachache watende kwa niaba yetu huku tukibaki "yatima, watazamaji, hatuna la kufanya, n.k." baada ya kukabidhi madaraka yetu?

Leo hii sio tu Rais bali pia Makamu wake, Waziri Mkuu, Spika, Jaji Mkuu, na Naibu Spika wana kinga za kutoshtakiwa wakiwa na hata baada ya kutoka madarakani! Pengine, kwa Katiba hii, huko tuendako list ya wenye kinga ikaongezeka; well, tuombe ikiwezekana wananchi wote wawe na kinga za kutoshtakiwa kama wao walivyo nazo. Aliyekuwa "amelala" na aamke sasa!

Apumzike kwa amani Beatrice Kamugisha angeidadavua vizuri sana hii mada!
 
Mungu mkubwa!!!!
 
Nakubaliana na muelekeo wa haya mawazo.
Tunashindwa kuiboresha Katiba kwa ajili ya mustakabali wa Taifa , lakini tunaibadili Katiba kuwanufaisha viongozi, hii si sawa.
 
Amini nakwambia mkuu ikitokea upinzani umeshika dola hakuna atakayeshughulika na katiba .
 
Binafsi sitaki upinzani kuchukua nchi, lakini nataka Katiba itengeneze mifumo imara ya kutekeleza uendeshaji wa nchi.
Hata Rais akifanya kosa la wazi, sheria ziwepo kurekebisha makosa.
 
Ni wazi sasa hivi kwamba Katiba imekuwa ikifanyiwa maraekebisho ya mara kwa mara, kwa convenience ya watu na siyo manufaa ya moja kwa moja ya nchi.

Serikali ilipitisha miswaada na kupitisha Bungeni merekebisho ya Katiba hivi karibuni ili viongozi wa juu kabisa akiwemo Rais, Makamu wa Rais, Spika, Makamu wa Spika Mwanasheria Mkuu.

Hapa dhana ya uwajibikaji katika madaraka inapotea.

Sasa sisi wananchi tunapodai uwajibikaji kikatiba, kama mmoja wa waliopo juu watafanya jambo kinyume na sheria, haki itapatikana wapi?

Hii Katiba tuliyonayo tukiendelea kuisuka suka kuwa kwa convenience ya watawala, hilo si jema kwa mustakabali wa nchi.

Na hili tunalisema hata sisi wana CCM maana tuliyoyaona Awamu ya Tano yanatosha.

Katiba iwe kwa manufaa ya wananchi, si watawala.
Kuna majinga flani ndani ya ccm yanapinga katiba mpya
 
Binafsi sitaki upinzani kuchukua nchi, lakini nataka Katiba itengeneze mifumo imara ya kutekeleza uendeshaji wa nchi.
Hata Rais akifanya kosa la wazi, sheria ziwepo kurekebisha makosa.

Katiba ikibadilika uwezekano wa ccm kuendelea kukaa madarakani haupo. Kinachoifanya iendelee kuwepo ni hii katiba maana haina ushawishi tena. Ukiona ccm hawataki katiba mpya si kwa bahati mbaya, kwani matokeo kwenye uchaguzi huwa wanayajua yanakuwaje.
 
Back
Top Bottom