Hata vichaa wanapenda...Nimeshuhudia

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,364
11,150
Familia yetu iliwahi kuishi jirani na familia ya mama na bibi mmoja miaka ya 90.Mama yule alikuwa na mtoto mwenye ulemavu wa akili (zamani tunaita kichaa)......Kwa kuwa tulikuwa wadogo tulikuwa tunamtania sana ingawa akikasirika vurugu la mawe linaanza.

"Kichaa" akawa mtu mzima kama miaka 25, wazazi wakamtafutia mke kijijini.....ilikuwa ngumu lakini kwa kuwa bibi ana vijisenti (nyumba na kilabu cha pombe), akampata binti akalipa mahari na harusi ikafanyika.

Hivi sasa yule kichaa ana watoto watatu copiraiti na maisha yanaenda......Ngoma akizuka mtaani mnaweza kumtania vitu vingi san lakini inapofikia kumtania kuhusu mke wake (mambo ya chumbani),kwanza anaona aibu lakini mkizidi analianzisha.....Mtapigwa na mawe mpaka mkome.

Jamani mapenzi hayana macho!! msione watu wanalia.....
 
Teh huyo kichaa chake hakikuwa kikali aisee
Kuna wengine moto wao noma haelewi kitu
 
Umekaa ukafikiri wee ukaona hapa jf ndo unaweza ukaweka uongo wako na watu wakakusapoti kwa huo uongo usioeleweka, ucjue waloko humu jf ni ma great thinker!
 
Hata KUPENDA ni aina ya kichaa, kwa hiyo kama na wewe unamonea wivu mtu wako una elements za kichaa pia.

Mtu akiwa na excessive wivu wa mapenzi unakuwa ni PATHOLOGICAL ambao unapelekea mtu kuwa na IRRATIONAL reasoning. Hicho ni kichaa tofauti hapa ni degree ama intensity
Kwa hiyo usimcheke yule kichaa na wala usishangae as no one is free from craziness or mania.
:A S wink:
 
Umekaa ukafikiri wee ukaona hapa jf ndo unaweza ukaweka uongo wako na watu wakakusapoti kwa huo uongo usioeleweka, ucjue waloko humu jf ni ma great thinker!

Sijawahi kuwa mpuuzi kiasi hicho kutunga uongo.....Inashangaza unajiita great thinker halafu una mashaka na mtu ambaye hujataka kumfahamu...pitia post zangu
 
Teh huyo kichaa chake hakikuwa kikali aisee
Kuna wengine moto wao noma haelewi kitu

Nafikiri mapenzi ya familia yalimfanya kutulia kidogo...lakini anapiga sana kazi za nyumbani (si ngono) kifupi si mvivu
 
Hii ni taarifa au?
Hatujabisha mbona?

Konnie bwana, ni story ya kweli sina upuuzi wa kudanganya hapa JF....NI majirani zetu hao miaka hiyo na tulikuwa tukicheza sana kwenye viwanja vyao hasa kombolela na mchezo wa kujificha...
 
Nafikiri mapenzi ya familia yalimfanya kutulia kidogo...lakini anapiga sana kazi za nyumbani (si ngono) kifupi si mvivu
Ok kwa namna hiyo kichaa chake kitakuwa kinapanda na kushuka so kikitulia anakuwa na hamu ya mapenzi na kuelewana
Nafikiri hata kwa vichaa wa kawaida kuna wakati huwa wastaarabu sana....hujawahi kuwaona?
 
Hata KUPENDA ni aina ya kichaa, kwa hiyo kama na wewe unamonea wivu mtu wako una elements za kichaa pia.

Mtu akiwa na excessive wivu wa mapenzi unakuwa ni PATHOLOGICAL ambao unapelekea mtu kuwa na IRRATIONAL reasoning. Hicho ni kichaa tofauti hapa ni degree ama intensity
Kwa hiyo usimcheke yule kichaa na wala usishangae as no one is free from craziness or mania.
:A S wink:

Kilichokuwa kinatushangaza nyakati zile ni vipi mtu kama huyu anaona wivu? halafu tunaulizana wanafanya vipi yale mambo yaleee
 
Nafikiri mapenzi ya familia yalimfanya kutulia kidogo...lakini anapiga sana kazi za nyumbani (si ngono) kifupi si mvivu
Huyo basi ana afadhali sana...kuna vichaa wengine wao ni kurusha mawe mwanzo mwisho hawajali wewe ni nani wala nini na wengine wao ni kubeba makopo....hope huyu ana afadhali sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom