Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,325
- 152,136
Walipotangaza kupunguza PAYE kutoka asilimia 11(kama sikosei) mpaka asilimia 9 watu walishangilia sana utazani punguzo hilo la asilimia 2 linahusu kila mfanyakazi na kwamba ingesaidia sana watumishi.
Siki chache baadae serikali hiyo hiyo iliodai imetoa punguzo ili kumsaidia mtumishi ikaja na nyongeza ya makato ya Bodi ya Mikopo kutoka asilimia 8 mpaka 15.
Wakati huo huo hela zote hizi zikikusanywa zinaenda kwanza kuwekwe kwenye kapu moja pale BOT kabla ya kuzisambaza na zote ni mali ya serikali.Wanavyozigawa wanajua wenyewe kwahiyo wakiamua kujifidia kupitia hiyo nyongeza ya makato hakuna anaejua.
Watu huwa wanashangili bila hata kutafakari kwanza na sijui watu hawa huwa wanakuwa wameandaliwa kushangilia maana mimi sielewi kabisa.
Jana kuna kodi zimefutwa na zingine kupunguzwa ila zikafidiwa kwa kuongeza kodi kwenye mafuta ya petroli na kwenye vinywaji.Yaani badala ya kubuni vyanzo vipya vya mapato kufidia kodi hiyo iliyopunguzwa, wao wakaongeza mzigo wa kodi kwenye bidhaa nyingine ambayo tayari nayo inatozwa kodi huku bidhaa yenyewe ikiwa ni nyeti kabisa na watu wakashangilia!!.
Leo hii kuna watu wanatumia magari tarehe za mwisho wa mwezi baada ya kupata mishahara na ikifika katika ya mwezi wengine hupaki magari kisa wanashindwa kumudu kununua mafuta na wengine hupunguza kabisa matumuzi ya magari yao.
Sasa ukiongeza kodi na bei ya mafuta ikapanda,watu hawa sio ndio watazidi kupaki magari na wakipaki magari au kupunguza mizunguko hiyo kodi unayotarajia kukusanya kutokana na mauzo ya petroli itaweza kweli kufidia hilo pengo?
Bila kubuni vyanzo vipya vya mapato na kila siku tukabaki na kucheza na vyanzo vile vile,tutabakia na kuwa na bajeti kubwa za kisiasa kwenye makaratasi lakini kiuhalisia inakuwa hamna kitu na bajeti hizi zitakuwa hazitekelezeki kama ambayo zimekuwa hazitekelezeki miaka yote.
Hii ni Bajeti ya kung'ata na kupuliza ila itang'ataza zaidi kuliko kupuliza utekelezaji ukianza.
Nadhani wanaoshangilia ama huwa hawatafakari au huwa wanaandaliwa kufanya hivyo kwasababu za kisiasa.
Time will tell.
Wanasema sisi tunapinga kila kitu lakini wanasahau kuwa wao wanaharibu kila kitu.