ni ngumu kidogo kuelewa kama haukuwa eneo la tukio au kumsikiliza jamaa akielezea kwa njia ya video
Ipo hivi huyo mhandisi wa kivuko alijifungia ndani ya hicho kivuko upande wa karibu na injini ambapo kiuhalisia maji hayakuingia, sasa ile siku ya pili ya uokoaji ndio wakasikia sauti mtu anagonga, lakin kulikuwa na upenyo mdogo ambao hakuweza kupita, kwahiyo wakatumia huo upenyo kuwasiliana nae na pia kumpa chai maana alikuwa na njaa ya siku mbili huku wakifanya jitihada za kuvunja na kwenda kumuokoa.