ujue kuna vitu vingine kuvisema/kumwambia directly ni noma so chance kama hizi zikitokea natumia humo humo
Wana MMU
Nawasalimia sana, jana nimesoma humu vijimambo nikacheka! hili jamvi haliishi mambo!
Kwa mfumo wa maisha ulivyo sasa, wanawake nao wamekuwa na ajira za kuajiriwa au ajira binafsi. Na misingi hiyo wanawake hao hujikuta wana pesa ya kujikimu au na hata ya zaidi. Wanawake hawa hujikuta wana au supply mahitaji ya nyumbani mengi au wanajazilizia yanayoupungua kutoka kwa mume!Ni jambo jema kwani linapunguza ukata kwenye familia na misongo ambayo inesababishwa na ukosefu wa pesa.
Pamoja na hivyo, dhana hii isipoangaliwa vyema huleta shida kwenye mahusiano ya mume na mke. Kwa kuona hivyo wanaume wengi hujikuta wakiridhika na ile hali kufikiri kuwa mkewe ana pesa hivyo kumpa zile tu matumizi ya nyumbani na kuendelea na maisha ya ujumla jumla.
BIG MISTAKE
Ni hatari sana hiyo kwani mwanamke ana vinasaba vinavyotaka apendwe na kuwa cared na mumewe. So hata kama mkeo ana pesa, usiache kumpelekea vijizawadi kwa mfano nguo, perfume, hela yake ya pocket money ya saloon, fuel na unamwambia kuwa wife hii ya wkend saloon ee mpenzi! Pamoja na mwanamke kuwa na uwezo wa kufanya mambo hayo yote, lakini anapofanyiwa na mume huvipa uthamani wa tofauti sana na kufurahia zaidi. Usishangae mkeo akipenda kutumia zaidi nguo uliyomnunulia hata kama ana uwezo wa kununua! Kuoa ni jambo moja na kutunza mke ni jambo lingine, muhimu, la maana, na linalolipa!
unazungumzia pipi? pipi sh mia eti ? wanaume wa siku hizi wabinafsi sana.baba zao hawakuwa hivi sijui wametoa wapi hizi tabia za kichoyo hivi....sasa kama hata pipi hupati si umuache? kama mtu hakuthamini wa nini sasa?
Smile mume haachwi kivyepesi hivyo, unavumilia kuna siku atajifunza, na amfanyie.unazungumzia pipi? pipi sh mia eti ? wanaume wa siku hizi wabinafsi sana.baba zao hawakuwa hivi sijui wametoa wapi hizi tabia za kichoyo hivi....sasa kama hata pipi hupati si umuache? kama mtu hakuthamini wa nini sasa?
Kwani umeongelea wapenzi au wanandoa? Nijuavyo mimi na ndivo ilivo kwangu " hakuna changu wala chake" budget inayopigwa ni ya familia yeye na mimi ni sehemu ya familia hivo budget yake ya mwezi inafahamika wakati wa kubudget. Baada ya hapo vizawadi itategemea na mishemishe zangu. Otherwise pato lake na langu kwa ujumla ni pato la familia.
naendelea kuisoma.........................
naunga mkono hoja hata kama nina pesa na kazi nzuri kunitunza ni lazima.Lakini wanaume wa kibongo wakiona umeingia ofisini tu zile allowance zote anakata afu ataanza kukukopa.Mpenzi wangu najua utasoma hapa naomba jirekebishe maaana na wewe hii tabia umeshaianza natamani kukwambia ila ntaanzaje?Ahsante kwa hii mada nimefikisha ujumbe zile allowances naomba zirudishe jamani.Naanza kupata mawazo labda kuna mwingine unampa
^^
There you come royna zawadi ni jambo jema sana lakini pesa yake inawekwa kundi gani katika bajeti ya familia?
^^
Hahahaha naona message delivered,kazi kweli kweli,Ila nadhani a man should be a man regardless mpenzi wake anafanya kazi,being a man is to handle all responsibilities.