hata baadhi ya wenyewe hawako serious, vipi wengine tuwe?!!!

hata baadhi ya wenyewe hawako serious, vipi wengine tuwe?!!!

PAPAKINYI - SJUT 2013

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
367
Reaction score
251
kuna thread zinazotupiwa humu zikilaumu kusahaulika kwa haraka kwa suala la tundu lissu....si mbaya, lakini kwa mtazamo wangu, hii inaanzia kwa wenyewe hukohuko au niseme kuwa hata wao wenyewe wanalifanyia dhihaka tu jambo hili....nitatoa mfano mmoja, ukikutosha sawa na usipokutosha utatafuta mingine wewe mwenyewe, ukiuafiki sawa na usipouafiki pia sawa lakini utasimama kuwa ni kweli tupu;

juzi kati mh. sugu alikuwa anachangia bungeni. alisema mambo kadhaa ambayo sikatai kabisa kuwa ni ya msingi tu kwa muskabali wa nchi yetu....aligusia elimu kidogo na kumlalamikia mama ndalichako kwa kumaliza karatasi n.k. lililonigusa na kunishangaza kidogo na ambalo linaendana na title ya thread yangu ni pale alipokuwa anazungumzia kuminywa kwa demokrasia. kiini cha mshangao wangu ni pale alipoutolea mfano wa kushambuliwa kwa risasi kwa watu wanaokosoa serikali KWA MASIGHALA (MASIHALA?/DHIHAKA) kubwa sana, kinyume na uzito wa suala lenyewe...ngoja nijaribu kunukuu,...

'.....tukisema mnatuvizia huko nje na kutuzimisha na tyuuu tyuuu', mwisho wa kunukuu. wabunge wote waliangua vicheko huku mwenyewe akiachia tabasamu mwanana kabisa!!!

hii ni dhihaka kubwa sana kwa suala kubwa kama lile na ndo maana sioni ajabu watu wengine nao wakilichukulia kiutani tu sababu wenewe, tena waheshimiwa, wanafanya hivyo.

naomba kuwasilisha!
 
Back
Top Bottom