Hasira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hasira

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by salustian, Jul 19, 2011.

 1. s

  salustian Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  USIKUBALI HASIRA IKUANGAMIZE.
  Katika maisha kuna nyakati mtu au kitu kimekukasirisha kupita kiasi.Wote huwa tunakasirika. Ni kitu cha kawaida kukasirika. Akili na mwili ndivyo vilivyo. Lakini hasira kupita kiasi hubomoa, huangamiza na huaribu starehe zote za maisha. “Usiende kulala ukiwaka hasira, simama na ishinde” Phyllis Diller aliwaasa wanawake katika kitabu chake kinachoitwa Phyllis Diller’s House Keeping Hints (Dokezo za Phyllis Diller za Utunzaji wa Nyumba) cha mwaka 1966 wakati wameudhiwa na waume au watoto wao.

  Katika hasira lazima kuna mabishano na chanzo chake siku zote si jambo jema. Ni kama kutupa jiwe kwenye mzinga wa nyuki. Tawala hasira, ikiwezekana zuia isitokee.Mara nyingi matokeo ya hasira huwa mabaya kuliko hata kilichosababisha hasira.

  Kuna msemo wa Watamili unasema hasira kali inaangamiza kuliko upanga. Tumeshuhudia wazazi wakiwaua watoto wao kutokana na hasira. Hakuna ambaye hajawahi kujuta maishani kwa matokeo ya hasira zake.

  Sekunde moja ya kuchelea kukasirika humwepusha mtu siku mia za majuto, ni msemo usiopingika. Shakespeare alisema mwenye hasira humjeruhi hata rafiki yake mpenzi.

  Wagiriki waliamini kuwa Miungu ikitaka kukuangamiza ilikuwa ikikukasirisha kwanza ili upoteze hekima kasha ujiue mwenyewe. Waliamini kuwa yeyote alieweza kukukasirisha alikuwa na uwezo wa kukushinda katika vita.

  Kila unapokasirika unamwaga sumu katika mishipa yako. Hasira huondoa busara na huonyesha upande wako wa pili usioufahamu. Kuwa na hasira kupita kiasi ni kama kuvua nguo hadharani. Kila unapojawa na hasira mwili wako hutenda maovu. Mwili haufanyi maamuzi ya hekima kwenye hasira, hufuata silika tu. Wakati wa chuki, maudhi, wasiwasi, matendo yote hasi hujaa katika moyo, akili na mwili. Usikubali hasira kupita kiasi kukukosesha heri na afya njema.

  Wengine hupata hasira haraka na kwa kiwango cha juu kupita wengine, wengine hawaonyeshi hasira kwa namna inayoonekana wazi, bali mara zote huwa na chuki na watu wa kulalamika. Waliokasirika si mara zote watalaani na kupigana, wanaweza kujitenga na jamii, wakawa wakiwa na wapweke hata wakaugua mwili.

  Watu wanaokasirika haraka kwa kawaida huwa hawawezi kuvumilia matatizo, hujisikia kuwa hawatakiwi kusumbuliwa au kuudhiwa.

  Ni vitu vingi hufanya watu wakasirike. Moja inaweza ikawa genitiki au saikologia. Kuna ushahidi kuwa watoto wengine huwa na hasira, utukutu, wakali tangu wakiwa wadogo kabisa. Sababu nyingine inaweza ikawa kijamii, kimazingira na kiutamaduni.

  Hasira mara nyingi huchukuliwa kama kitu kibaya katika jamii, tunafundishwa kuonyesha chuki, mawazo mazito au namna nyingine ile ya mtazamo lakini si hasira. Matokeo yake ni kwamba tunashwindwa kujifunza namna ya kukabiliana na hasira kwa njia iliyo sahihi.

  Maisha ya familia vilevile huchangia kutawala hasira. Mara nyingi wanaokasirika haraka hutoka katika familia sizizo na mshikamano, zenye matatizo na magomvi ya mara kwa mara hivyo hawajifunzi namna ya kuwasiliana vyema.
  Lengo liwe namna ya kuizuia na kutawla zaidi hasira kwa namna inayofaa.

  Hatari hapa ni kuwa hasira kupita kiasi inaweza kuchukua sura nyingine kama mtu akishindwa kuitawala na kusababisha shinikizo la damu, vidonda vya tumbo na hata magonjwa ya akili. Ukibakia katika hasira ni kama kushikilia kaa la moto kwa nia ya kumtupia mtu mwingine; NI WEWE NDIYE UTAKAYEUNGUA.
   
Loading...