Hashim thabeet atemwa NBA


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,863
Likes
8,686
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,863 8,686 280
Timu ya Memphis Grizzlies inayoshiriki ligi Kuu ya kikapu ya NBA, imempeleka mchezaji wake wa kati Hasheem Thabeet kwenye timu ya Dakota Wizards inayocheza ligi ya wachezaji wanaochipukia ya NBA Development League.
Thabeet, mwenye urefu wa futi 7 na inchi 3, ambaye alimaliza akiwa wa pili kwa ubora katika mchujo wa kuwania kuingia ligi kuu ya NBA kutokea vyuoni, ameshushwa daraja ili akajifue upya baada ya kuwa na wastani mbovu wa kufunga pointi 2.5, kuwahi ribaundi 2.9 na kuzuia 1.1 katika mechi 50 alizocheza. Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya chuo kikuu cha Connecticut, alifunga pointi 10 ambazo ndizo pointi zake nyingi zaidi katika mechi moja tangu atue NBA Januari 2 katika mechi dhidi ya Phoenix Suns.
Thabeet ameonekana kuwa ni mchezaji anayehitaji kujifunza zaidi kuboresha uwezo wake, lakini kutokana na mjumuisho adimu wa urefu wake na wepesi uwanjani, vilimfanya apewe nafasi kwenye kikosi dhidi ya wachezaji kama Tyreke Evans, ambaye alichezea Chuo Kikuu cha Memphis, Stephen Curry na James Harden.
Grizzlies hivi sasa imekuwa ikimtumia ikimtumia mchezaji kutoka Irani, Hamed Haddadi, ambaye yuko katika mwaka wake wa pili tangu atue NBA, akiwa kama mchezaji wa akiba wa nafasi ya mchezaji wa kikosi cha kwanza, Marc Gasol.
Thabeet, mwenye umri wa miaka 23, amekuwa ni mchezaji wa kwanza aliyeingia NBA kwa ubora wa juu zaidi kutupwa kwenye ligi ya "wanaochipukia" wa NBA. Mchezaji wa Portland, Martell Webster, ndiye aliyekuwa akiishikilia rekodi hiyo tangu mwaka 2005. Hata hivyo, Webster yeye aliingia NBA akishika namba 6 kwa ubora, wakati Hasheem aliingia akiwa bora zaidi kwa kushika namba 2.

CHANZO: NIPASHE
 
TANMO

TANMO

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Messages
8,957
Likes
334
Points
180
TANMO

TANMO

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2008
8,957 334 180
Kwa hiyo ina maana akipanda kiwango watamrudisha moja kwa moja NBA au itamlazimu kupitia tena kwenye mchujo?
 
Ndjabu Da Dude

Ndjabu Da Dude

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2008
Messages
4,015
Likes
703
Points
280
Ndjabu Da Dude

Ndjabu Da Dude

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2008
4,015 703 280
So much about last year's hype of dude being selected as NBA's 2nd draft pick. Some in here will exclaim "Told you so!" Goes to show dude may have the right genes but that clearly ain't enough for him to make it in the major league. Dude's definitely down for now, and may well be on his way out.
 
Kang

Kang

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2008
Messages
5,307
Likes
814
Points
280
Kang

Kang

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2008
5,307 814 280
Kwa hiyo ina maana akipanda kiwango watamrudisha moja kwa moja NBA au itamlazimu kupitia tena kwenye mchujo?
Anarudi moja kwa moja.
Hii sio kitu kibaya sana kama watu wanavyofikiri, maana jamaa anahitaji minutes, na akiwa Grizzilies sio rahisi kuzipata right now. Bora aende D-League apate experience zaidi, naamini atarudi better then ever.
 

Forum statistics

Threads 1,236,240
Members 475,029
Posts 29,251,215