Hashiki mimba nataka kumtimua

Hashiki mimba nataka kumtimua

manSniper

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2015
Posts
814
Reaction score
683
Mimi ni kijana na 28 tatizo nimeoa mwanamke mwaka wa 3 nilimkuta ana mtoto na mimi nilikua na mtoto wa nje sasa tatizo nilikuta anatumia sindano za uzaz wa mpango nilimsihi aache akaacha.

Sasa napiga hashiki mimba alianza kuhisi mimi mybe natatizo nilisingiziwa mtoto niliamua kuchepuka nikatafuta dem akababa mimba sasa ana mtoto wa kike nilimweleza ilimuuma sana akaniomba nimpeleke hospital akakutwa mirija ya uzazi imeziba.

Nilitumia gharama kubwa sana sasa ni miezi 7 hashiki mimba, naumia sana wazazi na ndugu wanalalamika eti kama vipi nichukue mmoja kati ya hao niliowazalisha nioe mmoja wao.

Naombeni ushauri bila matusi
 
Ongeza juhudi tu mzee utafanikiwa,ushauri ni kuwa acha kufanya ile kitu,muoe then nakushauri uendelee na yale mambo yetu huku ukimuomba Mungu atakusaidia utapata mtoto ila sasa hivi hata nikikushauri uombe Mungu itakuwa kazi bure maana hiyo ufanyayo ni zinaa tu.
 
subiri.... Hacha kuchukua maamuzi ya haraka na yasiyo na maana yeyote. Itaweza kuchukua muda mrefu... Nakushauri kapate ushauri kwa wataalamu wa afya ya uzazi.
 
Mirija kuziba ni tatizo linalotatulika na hapo lazima uingie gharama tena ya kutosha tu, kama unataka vya bure mtibu wewe. Ukitaka suluhu nicheki kwa 0686907486, 0718265581
 
Hashiki mimba AU wewe hutoi mimba? Tafuta majibu ya hilo swali kwanza
 
manSniper

1,Ww una uhakika gan kama hao watoto hujasingiziwa?....
2,wakat yy ameenda kupima hospital na ww ulipima?
3,Emu jifanye mwanamke kwa dk 3 alafu chukua nafasi ya huyo mwenza wako, je unajisikiaje kwa maneno yako?
4,Kama hao watoto wa nje ni wako je mapigo uliyokuwa unapiga kule ni sawa na huku? Isije ikawa unapiga kisharobaro au kibongofleva badala ya kupiga ki hip hop.
 
Last edited by a moderator:
manSniper

Sasa kama una watoto si mlee hao? Una lako jambo
 
Last edited by a moderator:
Matatizo ya afya ya uzazi ni changamoto kubwa kwa maisha ya ndoa. Inabidi uwe jasiri na mtambuzi na mchambuzi wa hali zote kama unataka kuwa na furaha. Tunabidi mjiridhishe ninyi mlio kwenye uihusiano badala ya kuwaridhisha kuwafurahisha wengine. Kila mtu na mwenzi wake wanatakiwa waishi maisha yao badala ya kuishi maisha ya ndugu au ya marafiki. La muhimu ni kumwona daktari kuwapima afya zenu na kupata matibabu yanayohitajika.

Kila la heri katika kufanya uamuzi mgumu. Kumuacha intaonyesha humjali!
 
manSniper

Suala hili ni gumu sana kwa sababu kuu 2:

kwanza ni malengo ya ndoa/mahusiano ya kudumu. Hapa kuna mambo ya kujiuliza je mlipoanza mahusiano, ambayo baadae yalipanda mpaka ndoa, matarajio yalikuwa nini? Mtoto ni moja ya nguzo kuu na kiunganishi cha ndoa,je mliwahi kulizungumzia ikiwa mtoto hatapatikana? Nyote mna watoto je wanaweza kutosheleza kama mtashindwa kupata wemgine?

2. Mtazamo wa wazazi na jamii inayokuzunguka: Hapa najua ndiyo kwenye mtiti maana kwa mila za kiafrika ndoa maana yake WATOTO ndiyo maana mababu zetu toka asili walioa wake wengi ili kupanua familia na kuendeleza ukoo.

Hivyo inabidi ufanye kazi ya ziada kuwashawishi kuendelea na mke baada ya miaka 2 bila mtoto! Hata pale ambapo wenyewe kwa kupendana kwa dhati na kukubali kuishi na hali hiyo ni kazi ngumu sana kuhimili pressure from telatives and friends. Nyinyi mna bahati tayari mna watoto, je ingekuwa nyote hamna hata wa kusingiziwa?
 
Last edited by a moderator:
Bwanae maisha yako na mkeo hayatakiwi kuingiliwa na ndugu kwa sababu hiyo hata kama msingekua na watoto kabisa hayawahusu ,wewe endelea kumpenda na kuishi na mkeo Mungu atajalia mtoto atapatikana kwa wakati muafaka hao ndugu wssikuzingue.
 
Jibu sahihi ni wewe kuleta matokeo ya sperm analysis......

Una uhakika gani kama mtoto wa huyo binti ulozaa nae ni wako? Mwanamke ndie oekee mwenye kusimama na kusema huyu ni mtoto wangu maana yeye ndio mbeba mimba.

Pia kabla ya kuoa.... lengo lenu lilikuwa nini?

Mlipoapa kwa shida na raha unajua ilimaanisha nini?????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom