Hasara ya vitabu vya TIE

Hasara ya vitabu vya TIE

Teleskopu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2017
Posts
703
Reaction score
768
Jana 9-10-2017, katika kipindi cha “This Week in Perspective” – TBC – kinachoendeshwa na Adamu Simbeye, waliongelea kuhusu Vitabu Vibovu vilivyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE).

Kati ya mambo yaliyonigusa ni gharama iliyotumika kuandaa vitabu hivyo vibovu.

Profesa Galabawa wa UDSM alisema kuwa, TIE wametumia:

ZAIDI YA BILIONI 144 😱😱😱😱😱

kuandaa vitabu hivyo ambavyo sasa havina thamani yoyote kuweza kutumika shuleni. Inabidi, ama vitupwe au kuchomwa moto.

Waziri Mkuu wetu alipoulizwa bungeni juu ya nini kinafuata, alisema:

- vitabu hivyo vinaondolewa shuleni,
- TIE wanaajiri wafanyakazi wapya wenye utaalamu,
- makosa ya vitabu yatarekebishwa. 🙁🙁🙁🙁

Kwa nini serikali inataka kurudia makosa yaleyale?

Acheni sekta binafsi ifanye kazi hiyo.

Serikali iwe SERIOUS kwenye kusimamia viwango.

Sekta binafsi ikishaandika vitabu, serikali ndiyo iwe na usemi wa mwisho kusema, “Kitabu hiki kizuri, tutakitumia. Hiki ni kibaya hatukitaki.”

upload_2017-7-10_7-29-20.png
 
hakuna kipya kitakachoongezwa zaidi ya kukopy kwenye vitabu vingine vya zamani!
Ninachwaomba wasituondolee vitabu vya kingereza vyenye stori tamu vya ngugi wa thiong'o
 
Back
Top Bottom