Harusi za kifahari zapigwa marufuku Somalia

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_93561832_somaliawedding.jpg

Mji mmoja nchini Somalia umepiga marufuku harusi za gharama ya juu ili kuwashinikiza vijana zaidi kuoa.

Kamishna wa wilaya Mohamud Hayd Osman wa Bula Hawa karibu na mpaka wa Kenya waliambia BBC kwamba ni mbuzi wasiozidi watatu ndio wanaofaa kuchinjwa pekee ili kuwalisha wageni na kwamba sherehe katika hoteli hazitaruhusiwa.

Amesema kuwa mahari itakuwa chini ya dola 150 pekee.

Uamuzi huo unajiri baada ya maafisa kubaini kwamba takriban watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa hivi karibuni.

Kamishna huyo ameongezea kwamba gharama ya harusi, ukosefu wa ajira na kiangazi ndio maswala yanayowafanya watu kulihama eneo hilo.

Waandishi wanasema sio kawaida kwa familia ya bwana harusi kutumia takriban dola 5000 katika harusi nchini Somalia.

"Mafunzo ya kiislamu yanasema kuwa ndoa inafaa kuwa ya gharama ya chini, alisema Osman.

Hatua ya kupunguza matumizi kuhusu sherehe za kifahari pamoja na matumizi mengine baada ya ya maafisa kugundua kwamba ni kwa nini watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa mjini humo.

Wasichana walikuwa wanakataa kuolewa hadi pale kitita cha pesa kitakapotumika kwa dhahabu pamoja na fanicha, alisema.

Chanzo: BBC
 
Huku kwetu ukitaka kuoa unafikiria sana harusi kuzidi hata hyo mahar yenyewe,harusi ya milioni kumi ya kawaida sana,na hutoki hata na kumi hapo,tena usipokuwa makini utakuja kugongewa mlango honeymoon kuna vitu havijalipiwa
 
Maamuzi ya sherehe ya harusi yako iweje ipo kwako.
 
Siku hizi hata wadau wanalazimisha sana,kuna ndugu yangu alioa kwa kuminimize sana cost,aisee anachukiwa mpaka Leo,alikokwenda kuoa wakaanza kumtisha mwanamke kua mumeo atakuja kukusumbua sana,anaonyesha mkoloni,bahiri,anadharau nk,ila wabaishi poa tu,japo ukweni hawamkubali hata kidogo na DOA lilianzia kwenye harusi
 
Ndoa ni baina ya watu wawili kwa makubaliano yao... Na ukipata mwenza anaelewa sherehe na mbwembwe za party ni extra kikubwa ni ndoa hutapata shida. Duniani huwezi kuridhisha watu wote na kupendwa na wote. Kikubwa kwenye harusi yako do what pleases you two married couples basi. Tusikubali kuendeshwa na watu ktk kufanya maamuzi
 
Siku hizi hata wadau wanalazimisha sana,kuna ndugu yangu alioa kwa kuminimize sana cost,aisee anachukiwa mpaka Leo,alikokwenda kuoa wakaanza kumtisha mwanamke kua mumeo atakuja kukusumbua sana,anaonyesha mkoloni,bahiri,anadharau nk,ila wabaishi poa tu,japo ukweni hawamkubali hata kidogo na DOA lilianzia kwenye harusi

Hohoo!kwamba jamaa ana sifa ya uchoyo au ubanizi wa kutumia fedha au mali ambao kwa neno moja huitwa ubahili.Ila wanawake wengi hawapendi mwanaume anaebana sana uchumi.Wanataka angalau falsafa za kufuja mali zimakinike ktk familia.
 
Sababu kubwa ya kupunguza bei ya mahari ni kuwa wanaume wengi wa kisomali wamekufa vitani kwenye mapigano wanawake ni wengi mno wasio na waume.Wanachokifanya hao mfumo dume wa kisomali ni kuwa wameshusha bei ya wanawake ili wanaume wakware wachache wa kisomali wajinunulie wanawake wengi kwa bei ya kutuopwa wawaoe.Si tu wameshusha bei ya mwanamke sokoni lakini na utu wake pia.Wapuuzi wakubwa wanakuwa na tume ya bei kwenye mahari mbona hawaweki kwenye bidhaa zingine?
 
We jamaa vipi . Kumbe mahari ni malipo ya kumnunua mwanamke...!!!Makubwa!!!!
 
Hohoo!kwamba jamaa ana sifa ya uchoyo au ubanizi wa kutumia fedha au mali ambao kwa neno moja huitwa ubahili.Ila wanawake wengi hawapendi mwanaume anaebana sana uchumi.Wanataka angalau falsafa za kufuja mali zimakinike ktk familia.
yaaa mkuu,sio bahir ila hapendi harusi za kifahari
 
Kufikikilia sana kwa wabongo ni hasa kwa harusi zetu wakristo zina ghalama sana kuliko islamic
Do you know why? To Christians, marriage, like birth and death, is regarded as one-time event in life except very very rare cases. Kwa wengine unaweza ukaoa kadhaa halafu kama vipi ukaacha ukoa tena kisha ukaacha ukaoa tena kisha ukaacha ukaoa tena, ..., n-times.

Kuna m-mama mmoja tuko naye ofisini huyo mume aliye naye ni wa tano. Kwa utaratibu huu ni lazima shughuli ifanywe ya gharama ndogo else haitatekelezeka. Iko hivyo purposely japo kutokana na mabadilko ya kijamii duniani mambo yanaelekea kubadilika siku hizi.
 
Sababu kubwa ya kupunguza bei ya mahari ni kuwa wanaume wengi wa kisomali wamekufa vitani kwenye mapigano wanawake ni wengi mno wasio na waume.Wanachokifanya hao mfumo dume wa kisomali ni kuwa wameshusha bei ya wanawake ili wanaume wakware wachache wa kisomali wajinunulie wanawake wengi kwa bei ya kutuopwa wawaoe.Si tu wameshusha bei ya mwanamke sokoni lakini na utu wake pia.Wapuuzi wakubwa wanakuwa na tume ya bei kwenye mahari mbona hawaweki kwenye bidhaa zingine?
Hivi mwanamke ni kama bidhaa?
 
Kufikikilia sana kwa wabongo ni hasa kwa harusi zetu wakristo zina ghalama sana kuliko islamic
Gharama wanaitaka watu na sio ukristo... Unaweza ukafunga ndoa kanisani na ikaishia hapo,ni maamuzi yako
 
Thamani ya harusi ya Kikristo ni kubwa sana na ndio maana huambatana na sherehe kubwa... Hiyo ni toka enzi nipo mdogo huko vijijini sherehe za harusi zilikusanya kijiji kizima unaweza usiamini gharama hizo za enzi za mababu. Hata kama hapakuwa na card za mwaliko lakini ilikuwa ghali sana kulisha kijiji kizima kwa kila aliyehudhuria. Hii inaonesha umuhimu na unyeti wa tendo Takatifu la Harusi ya Kikristo. Ni one time event
 
we baba wawapi..!? utakuw wa TARIME nani alikwambie kuwa unapomtolea mahari mwanamke ndio tiar unakuwa ushamnunuwa...?? acha uzuzu...
Umequote kitu kisichokuhusu. Msome niliyemquote ndio utanielewa badala ya kukurupuka. Mimi nineshangaa jamaa anaesema "kupanga bei" nawe unatoka huko na mapovu juu.
 
Back
Top Bottom