Hizi ndio Sababu 7 za kwanini Marekani ilishindwa vita ya Vietnam

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Baada ya Vita vya pili vya dunia, Marekani ikawa nchi yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi ulimwenguni, na nchi hiyo iliamini kwamba jeshi lake pia lilikuwa na nguvu zote. Lakini baada ya kutumia pesa nyingi na nguvu kazi katika Vita vya Vietnam kwa miaka minane tu, Marekani ilishindwa na vikosi vya Vietnam Kaskazini na washirika wao wa msituni, Viet Cong.

Katika kuadhimisha miaka 50 ya kuwaondoa wanajeshi wa mwisho Marekani kutoka Vietnam (Machi 29, 1973), BBC iliwauliza wataalam wawili na wasomi kujua ni kwa nini Marekani ilipigwa na kushindwa katika vita hivy.
Vita baridi ilikuwa katika kilele chake.

Mamlaka za ulimwengu za Kikomunisti na za kibepari baadae zilikabiliana.
Ikifilisiwa na Vita vya pili vya dunia, Ufaransa ilijaribu bila mafanikio kuhifadhi makoloni yake huko Indochina. Katika mkutano wa amani, waligawanya Vietnam ya leo kuwa kaskazini ya kikomunisti na jimbo linaloungwa mkono na Kusini inayoungwa mkono na Marekani.

Lakini kushindwa kwa Wafaransa hakukumaliza mzozo katika nchi hiyo. Waliogopa kwamba ikiwa Vietnam itakuwa ya kikomunisti kabisa, ukomunisti ungeenea hadi nchi jirani. Na hilo ndilo lililoiingiza Marekani kwenye mzozo huo uliodumu kwa muongo mmoja na kugharimu maisha ya mamilioni ya watu.
Kwa hiyo jeshi lenye nguvu zaidi ulimwenguni lilishindwaje katika vita na waasi wataifa jipya lililoanzishwa katika Asia ya Kusini-mashariki?

Wataalamu wawili wana haya ya kusema:

Majukumu ya kivita yalikuwa makubwa sana
Kwenda upande wa pili wa dunia kupigana vita ilikuwa jukumu kubwa. Katika kilele cha vita, kulikuwa na zaidi ya wanajeshi 500,000 wa Marekani waliokuwa kwenye ardhi ya Vietnam.

Gharama ya vita hivi ni ya kustaajabisha. Ripoti ya mwaka 2008 kwa Bunge la Marekani ilisema gharama ya jumla ya vita ilikuwa dola bilioni 68.6 (zaidi ya dola bilioni 95 katika viwango vya leo vya fedha).

Lakini Marekani ilitumia zaidi ya mara nne ya kiasi hicho katika Vita vya pili vya dunia na hatimaye ikashinda. Pia walianzisha vita vya muda mrefu nchini Korea. Kwa hiyo hapakuwa na wasiwasi wa imani katika vichwa vya viongozi wa Marekani kuhusu matokeo ya Vita vya Vietnam.

Mwingine, waasi wa Viet Cong wakizunguka huku na kule kwenye misitu hiyo isiyo na maji na kufanya mashambulizi ya siri.

Vietman

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES


"Ni vigumu sana kwa jeshi lolote kubwa kufanya kazi katika aina ya mazingira ambayo majeshi ya Marekani yalilazimishwa kupigana," anasema Dk Midap.

"Maeneo mengi yalikuwa na baadhi ya misitu minene zaidi Kusini-mashariki mwa Asia."

Jambo lingine muhimu, kulingana na Midap, ni kwamba waasi waliamua lini na wapi mapigano yangefanyika. Baada ya mashambulio, wangerejea kwenye maeneo salama kuvuka mpaka wa Laos na Cambodia. Vikosi vya Marekani vilipigwa marufuku kuingia katika nchi hizo mbili.

raia wasio na hatia. Habari hizi zilikuwa zikiangaziwa kwenye TV na magazeti. Hii iliwatia hofu Wamarekani wengi na mitazamo yao ikageuka kuwa ya kupinga vita.

Maandamano makubwa yalianza kufanyika kote nchini humo.

Vietman

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mnamo Mei 4, 1970, waandamanaji wa amani wanne walipigwa risasi na Walinzi wa Kitaifa katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Kent huko Ohio.

"Mauaji ya Jimbo la Kent" yalilikoleza upinzani zaidi wa watu dhidi ya vita.

Inaelezwa takriban wanajeshi 58,000 wa Marekani waliuawa au kutoweka wakiwa vitani Vietnam.

Kulingana na Profesa Vu, hii ilikuwa faida kubwa kwa Vietnam Kaskazini: ingawa pia walipata hasara kubwa, walikuwa na udhibiti kamili juu ya vyombo vya habari vya serikali na ukiritimba wa utoaji wa habari.

"[Vietnam Kaskazini] ilikuwa na mfumo mkubwa wa propaganda. Walifunga mipaka na kuzuia upinzani wowote. Yeyote ambaye hakukubaliana na serikali kuhusu vita alipelekwa gerezani moja kwa moja."

ambao walikuwa wameandikishwa kupigania Vietnam Kusini.
"Baadhi ya utafiti ulifanyika nchini Marekani kulingana na kuhojiwa kwa idadi kubwa ya wafungwa wa kikomunisti wakati wa vita," anasema.

Vietman

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES


"Rand Corporation, Shirika la utafiti linaloshirikiana na Idara ya Ulinzi ya Marekani na jeshi la Marekani, lilifanya tafiti hizi juu ya motisha na ari ya wafungwa. Walitaka kujua kwa nini Wavietnam wa Kaskazini na Viet Cong wanapigana vita hivi. Na taasisi mbili zilihitimisha kwa kauli moja kuwa motisha ya wafungwa inatokana na uzalendo. . Yaani walitaka kuunganisha nchi na kuunda serikali moja."

Uwezo wa vikosi vya Kikomunisti kuendelea kupigana licha ya mauaji makubwa ya msituni labda ni ushahidi wa ari yao.

Vietnam kuwa nchi mbili."
"Kuwepo kwa wanajeshi 500,000 wa Marekani chini nchini Vietnam kulionyesha ukweli kwamba serikali hii ilikuwa tegemezi kwa wageni kwa kila njia," Dk. Midap anasema.

"Vietnam Kusini haikuweza kujenga mtizamo ambao ungewashawishi raia kwamba mapambano yalikuwa mapambano ya maisha na kifo."

Hili, anasema, linazua swali la iwapo hata ilikuwa muhimu kutuma wanajeshi wa Marekani katika nchi iliyojaa ufisadi.

"Tangu kuanzishwa kwake hadi kufa kwake [Jamhuri ya Vietnam] ilikuwa nchi yenye ufisadi sana," anasema, akiongeza kuwa "msaada mkubwa wa Marekani kutoka miaka ya 1960 hadi 1975 ulifanya ufisadi wa nchi kuwa mbaya zaidi. Ufisadi uliokithiri ulidumaza kabisa uchumi wa Vietnam Kusini."

"Wakati huo hakuna mtu ambaye angeweza kushikilia wadhifa wa kiraia au kijeshi bila kutoa hongo." Alihisi ilikuwa na athari kubwa kwa vikosi vya jeshi.

"Hii ilimaanisha kuwa Marekani haiwezi kamwe kujenga jeshi la kuaminika na lenye ufanisi la Vietnam Kusini," anasema.

"Kwa hiyo ilikuwa ni jambo lisiloepukika - na Rais Richard Nixon alitambua - kwamba wakati fulani katika siku zijazo wakati askari wa Marekani watakapoondoka na kurudi nyumbani, Vietnam Kusini ingeanguka mara moja."

akimaanisha kwamba Vietnam Kaskazini inaweza kutumia mbinu za kijeshi kama vile mashambulizi ya kujiua ambayo Vietnam Kusini haikuweza."

Kilichokuwa muhimu zaidi, aliongeza, ni kwamba licha ya uungaji mkono wa Marekani kwa Vietnam Kusini, hakukuwa na harakati za usaidizi wa kifedha na kijeshi kutoka Umoja wa Kisovieti na Uchina kwenda Vietnam Kaskazini.
 
Hakuna historia ambayo inachukiwa na wanasiasa wa Marekani kama vita ya Vietnam.

Ni historia iliyo jaa aibu kwa taifa la Marekani na ndio maana sasa hivi wanafanya kila wawezalo kuisaidia Ukraine ili kuhakikisha Urusi inashindwa vita hii ili aibu ya kushindwa na mataifa madogo wanaibebe wote..
 
Hakuna historia ambayo inachukiwa na wanasiasa wa Marekani kama vita ya Vietnam.
Ni historia iliyo jaa aibu kwa taifa la Marekani na ndio maana sasa hivi wanafanya kila wawezalo kuisaidia Ukraine ili kuhakikisha Urusi inashindwa vita hii ili aibu ya kushindwa na mataifa madogo wanaibebe wote..
Na hawasemi😂😂😂 sijapenda kwa kweli
 
Ili ushinde vita major factor unahitaji public support , alaf mengine kama technology , mafunzo n.k ndo yanafata , hata uwe na jeshi imara namna gani ukikosa support ya wananchi kwisha habari yako ,... Wananchi wakiamua kukusupport hata kama utazidiwa namna gani , matumaini huwa yapo , mpak adui atakimbia mwenyewe.....

Marekani vietnam alikosa public support sawa na afghanistan , yaan wakat wanajeshi wanapambana manung'uniko yalikuwa mengi sana Marekani , kuwa vijana wanakufa bila sababu yyte na bila faida , uungwaji mkono wa operation ulikuwa mdogo sana ,

Kitu kingine wavietnam walikuwa well organized , wakitumia guerrila warfare , hii ni mbinu au ni njia hutumiwa na watu ambao hawana mpango wa kukata tamaa ....
 
Hoja siyo msaada,hoja ni kushindwa Vita hivi karibuni tukiacha ya kale ya Vietnam,miaka 20,$trilions,Vita mmeshindwa,Taliban anatawala na silaha mmemwachia,mkaondoka mbiombio mkimuomba Taliban asiwashambulie
... sababu zilizopelekea US kuingia Afghanistan hazipo tena. Kwanini aendelee kubaki huko?
 
Back
Top Bottom