kumbe unatumia hela ya nani?!! ukiwaita wanakamati tu siku ya kwanza kabisa wanakuuliza "bwana mdogo unataka harusi, umeandaa shilingi ngapi?"..oooh, milioni mbili..."milioni mbili? yaani umetuita hapa unataka kuowa una milioni mbili?" unajivutavuta mpaka tatu (sijui umekopa umefanya nini utajua mwenyewe), michango inaanza, wale wanaokuchangia hawakupi bure hiyo pesa ndugu yangu, UNAKOPESHWA!! Kadi zitapoanza kuporomoka kila wiki mchango laki harusi ya mfanyakazi mwenza, mara ya jirani, mara ya nduguye rafiki utarejesha tu huo mkopo...kuwa uyaone! mimi nilishakataa zamani hayo mambo, kama ni harusi ya mwanangu sijui ya nani tunaweka harusi tunayoweza kuimudu bila michango, ufahari pembeni, waalikwa wa muhimu tu...kwisha!