Harusi ina umuhimu ?

KAIZER ,mahari elfu 20 ?! ,Wapi huko wanapatikana kwa 20.000 ,yaani mahari niliyodaiwa ya milioni mbili napata wake 100 ,aloo hebu nitumie walipo kwenye pm ,salaaleh ,yaani kama bahati naona inaelekea kuniangukia ,ila huku nikiwambia mahari hayo ya 20,000/- watanifukuza tu hawana chaguo jingine ,yaani ni kadi nne za mtandao wa simu za elfu tano tano . Pengine hao wana ugonjwa flani ,haiwezekani kabisa udaiwe fedha hiyo .yaani hapo hata sherehe nzima nitaihudumikia ,sihitaji ushirika wowote ule.

Kaizer inawezekana haujafika hapa Tz mida mwingi ,inaonyesha uliondoka wakati wa kipindi cha watu kutelekezwa geza ulole,siku hizi kama huna juu ya milioni na nusu basi inakuwa mbinde ,maana utaanziwa ,unajua hata fanicha siku hizi zimepanda ,vyombo ndio usiseme hizo milioni umetoa itabidi na sie wazazi tumuongezee mwenetu apate mambo ya nyumbani na atengeze nyumba yake ,unaletewa stori ndeeefu ,ukizubaa tu umeumia ,hizo feza huyo mtoto wala haioni ,yaani angalau unaweza kupanga na huyo mke kuwa baada ya harusi akurudishie japo nusu ya mahari.

hahahahaha Mkuu Mwiba unanivunja mbavu kweli..mi nimezungumzia katika muktadha wa dini, hususan ya kiislam, ambayo kwa jinsi ninavojua mahari ni haki ya mwanamke anayeoa, kwa hiyo akisema anataka 20,000, basi hakuna zaidi na hailzaimishwi, kwa hiyo we pangana na mchumbako!

Hayo ya fenicha na nini kwani huyo binti ndo ameshakuwa mtaji wa wao kupata fenicha, hivi ufisadi si ni pamoja na huu mkuu!

Njoo bara huku, kuna makabila wanaoza, wala huhitaji kutoa mahari maana wao wameshatajirika tangu zamani!
 
Mwiba hataki sherehe kwa kuwa huyo ni mke wa pili ama wa tatu, hivyo anaogopa kufanya sherehe ili asiwakere wale wake zake wa mwanzo.

Kwa ushauri tu mtafute mjane, hapo unaweza kuoa pasipo mambo ya sherehe... Lakini kwa huyo mwali sio rahisi bila sherehe!
 
Mwiba hataki sherehe kwa kuwa huyo ni mke wa pili ama wa tatu, hivyo anaogopa kufanya sherehe ili asiwakere wale wake zake wa mwanzo.

Kwa ushauri tu mtafute mjane, hapo unaweza kuoa pasipo mambo ya sherehe... Lakini kwa huyo mwali sio rahisi bila sherehe!

Na ndio huo mtihani nimepata yule mwali amekubali kuachana na kusoma ,na ndio nipo katika kutayalisha na kutafuta mipango ya kuvuka harusi ya sherehe, mi nilimwambia wahi kuolewa siku hizi kupata mtu akakuoa ni mtihani peke yake na kweli hata wazazi wake waliliona hilo ,waliinisabia kama nyumba ishilini hivi zina wasichana wameshaanza kupevuka na wengine iliwahi kutokea bahati ya kuchumbiwa ila waliwarudisha warume ,na sasa wamebaki na majuto ,mi nawambia labda serikali iliyowawekea kizingiti iwatafutie.Ila kwa sasa mwanamwali akijidai nyodo tu atavunda na kupevuka. Ata muhogo ukipevuka akuna anae utaka na wengine utasikia wakipiga makelele kuwa nyama ngumu kwa maana kuku limeshapea inabidi ulitafutie magadi ili kulilainisha ,hata hivyo bado walaji wataponda ,ukiangalia sana hata wale wazazi wanatafutiwa kuku wachanga wachanga. natumai uminielewa :D
 
aisee, pole sana!
kwanza kama unaishi dar mkuu kilo 3 haitoshi kwakweli, hata ukumbi hupati kwa kilo 3 ndani ya dar, atleast ungekua na kilo 5.
pili wanandugu usiwajaze, wengi miyeyusho tu, hawako serious hata kidogo na watakulostisha, tafuta marafiki zako wale wa karibu na ndugu wachache wenye akili, isitoshe kwenye kamati inatakiwa mwanakamati atoe hela ya uchakavu, sasa hapo kwenye uchakavu kuna wengine wanakunywa bia 5 halafu wanatoa 2000 upumbafu mtupu
icon8.gif
!, kunywa kadri ya pesa yoko bana.
wewe mbona unacomplicate mambo
kikao cha harusi kinahitaji ukumbi
sebuleni tuu nyumbani inatosha
kwa nini watu wanye bia tano, bia moja tu inatosha
tatizo watu wanageuza vikao kuwa mahali pa ku socialize
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom