Harusi hakuna kisa huna pesa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Harusi hakuna kisa huna pesa!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babu Lao, Apr 23, 2011.

 1. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kijana Najab ambaye leo hii usiku wa saa mbili alikuwa afunge ndoa na mchumba wake wa takriban miezi minne hivi amefanyiwa ukatili wa hali ya juu kwa ndoa hiyo kuvunjwa.

  Kijana Najab ambaye anafanya kazi katika kampuni ya kutengeneza maji ya samawati tulivu iliyopo Mikocheni Light Industry karibu na ITV, amekuwa akijiandaa na siku hiyo kubwa tangu mwishoni mwa mwaka jana ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo makubwa nyumbani kwake, kununua furnitures na vingine vingi tu.

  Leo hii mchana mimi na wenzangu kadhaa tulialikwa karamu na Mama wa Najab aitwae Bhai Rukia katika kusheherekea ujio wa mke wa Najab. Tulipofika pale tukakuta wanaume watatu bila kujua nini kiliwaleta baada ya muda wakaondoka. Ndipo tukatanabahishwa kuwa wale waliotoka pale ni baba za mke mtarajiwa na wamekuja kwa mume mtarajiwa kukagua atakapoenda ishi binti yao, hii kali!

  Tukapuuzia mambo yale tukapata mlo kisha tukasambaa kwenda subiri muda wa kwenda kuoa ambao ulipangwa uwe saa 2 usiku katika msikiti Shadhiriya Kariakoo jijini Dar. Ilipotimu saa 1 usiku ndipo wale mabwana watatu wakarudi na kusema kuwa wameonelea harusi iahirishwe mpaka Bw Najab atakapokaa vema kifedha nk, walipobanwa sana ndipo wakasema wameona hawawezi kumtoa binti wao aende akae hapo kwani hapana hadhi ya mtoto wao kuishi.

  Kama ilivyo ada penye wengi hapakosi neno, inesemekana mmoja wa wale mabwana watatu waliofika mahala pale ndiye mchumba mpya na inasemekana FLUSI ipo na ana biashara lukuki nchini China. Kwa hiyo hivyo huyo bi harusi amepigwa mnada na mwenye dau kubwa ndio kapewa.

  Angalizo: Je ni haki kweli kumnyima mtu mke sababu hana pesa??

  Source: Arusi imeahirishwa! Sababu? Huna "njuluku" - Wavuti
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hapa mkuu hakutendewa haki kama si mke ndo alomtema baada ya kuona mme mpya ana fedha!!:sleepy:
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Bila pesa hakuna kinachoeleweka.....
   
Loading...