Habari I wana JF mdogo wangu anataka kufanya harusi budget yake ni 14,000000 hataki mchango wa harusi kwa mtu yoyote watu wa kuhudhulia 200. Je pesa hio itatosha. Waliohudhuria Kamati za harusi naomba michango yenu ya mawazo.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Shalom,....
Mosi,kwa uzoefu wangu ni kwamba usipowashirikisha waalikwa kwa ama njia ya kuimba michango au mipango ya maandalizi ya harusi,wengi huwa hawahudhiriihata kama utatoa mwaliko.
Pili,gharama kubwa za harusi huwa ni Chakula,vinywaji na mapambo.Gharama nyingine huwa ni fixed kama bei ya ukumbi,mc,music,dj....kwa.sasa bei ya dj mkali.kwa hapa dsm si chini ya Tshs 2.5mil.
Muhimu,ni kuandaa orodha ya wageni wote wanaotegemewa kualikwa.Waombwe kuthibitisha uwepo wao kwenye harusi hiyo kwa tarehe unayokusudia ili uweze kufanya mipango mapema pamoja na kufanya makadirio hasa ya chakula na vinywaji,uzuri hata vinywaji vikibaki bado kuna nafasi ya kuvirejesha kwa supplier ila atanunua kwa bei ya jumla.
Tofauti na Chakula ambapo kikiandaliwa hakirejeshwi endapo kama hakitatumika na hivyo huishia kuwa hasara.
Mwisho,kiasi hicho cha tshs 14mil,kinatosha sana kufanya harusi ya wageni 200.
Mpe hongera sana mdogo wako na Mwenyezi Mungu awajalie maharusi maisha ya mema yenye kheri na furaha ktk ndoa yao.
Kuoa na kuolewa ni jambo la kheri.
Wasalaam,
Mwenzetu
Sent using
Jamii Forums mobile app