Haruna Masebu alihitajika sana utawala huu wa Magufuli

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,229
116,840
Unamkumbuka Haruna Masebu?

Unakumbuka huyu jamaa wakati akiwa mkurugenzi wa Ewura aliambiwa na JK ashushe.

bei ya petroli....akamjibu live tena hadharani tu kuwa 'hakuna sheria inayompa mamlaka hayo' wakitaka wapitishe sheria kwanza.

Na baada ya sheria kupitishwa ndo Ewura ikawa na mamlaka ya kushusha bei na kupanga bei za mafuta...kushusha na kupandisha .'kwa mujibu wa sheria'...

Sasa watu wa aina siku hizi ni kama hakuna kabisa watu ambao sio waoga
wanaweza kuongea live sheria zinasemaje kwa swala husika bila woga
labda Benno Ndulu ingawa na yeye anasakamwa kwa kuongea tu ukweli sheria zinasemaje..

Leo nimemkumbuka sana Haruna Masebu.....mzalendo ,mchapakazi,asiye muoga kumwambia kiongozi wake ukweli.

Imagine kama IGP angekuwa anaweza kuwaambia wanasiasa tu ukweli kuwa katiba na sheria zinaruhusu shughuli za kisiasa na mikusanyiko ya kisiasa.....polisi haiwezi kufanya lolote wakitaka wabadili sheria.Na pengine kufuta kabisa vyama vya siasa.

Imagine Mkuu wa mkoa angekuwa na mtu anamwambia live 'agizo lako hili halipo kisheria' na kadhalika na kadhalika......labda matamko mengi ambayo hayana nguvu za kisheria yangekwisha.

Watu kama Haruna Masebu wanahitajika sana kipindi hiki.
 
Tatizo ni kwamba kwasasa watu wanamuogopa boss wao..hakuna hata mmoja anaweza kumkosoa.

Tulikuwa kwenye kikao flani..walimu wakuu wakauliza kuhusu nani analipa gharama za picha za usajili wa mitihani ya kidato cha nne..(maana waraka wa elimu bure umekaa kimya kuhusu swala hili).

Afisa elimu aliwaambia walimu wakuu wakae kimya maana ata yeye hajui..na alisema pia afisa elimu wa mkoa hana majibu na waziri alikaa kimya anaogopa kutoa tamko lolote maana anaogopa kumchukiza boss wa elimu bure.

Suala la picha lilisumbua sana kila mtu anaogopa kulisema yaani serikali haina hilo fungu lakini wanaogopa kuwachangisha wazazi.
 
Tatizo ni kwamba kwasasa watu wanamuogopa boss wao..hakuna hata mmoja anaweza kumkosoa..
tulikuwa kwenye kikao flani..walimu wakuu wakauliza kuhusu nani analipa gharama za picha za usajili wa mitihani ya kidato cha nne..(maana waraka wa elimu bure umekaa kimya kuhusu swala hili)
afisa elimu aliwaambia walimu wakuu wakae kimya maana ata yeye hajui..na alisema pia afisa elimu wa mkoa hana majibu na waziri alikaa kimya anaogopa kutoa tamko lolote maana anaogopa kumchukiza boss wa elimu bure..
swala la picha lilisumbua sana kila mtu anaogopa kulisema..yaani serikali haina hilo fungu lakini wanaogopa kuwachangisha wazazi..

Na wanavyoendelea kukaa kimya ndo mambo yanazidi kuharibika
 
Kwa huyu malaika ukimjibu hadharani kesho yake unatumbuliwa, bora wakae kimya ili aendelee kufanya makosa, kama ni namba tunaisoma wote
 
Kusema Kusema ukweli kunataka uhakika sana wa unachokisema na hiyo personality ya kusema ukweli sababu kusema ukweli pia ni tabia ya mtu nje ya utaalamu alionao
 
Mkuu The Boss, nikukumbushe vile vile majina ya viongozi wengine waliokuwa wanazingatia sheria, miongozo na kanuni siyo kutekeleza majukumu kwa mihemko na kumuogopa kiongozi wa ngazi ya juu. Wazelendo hawa ni:

(1) Professor G. V. Mmari: Vice Chancellor, Open University, Sokoine University, University of Dar Es Salaam wakati wa awamu ya 2 na ya 3
(2) Engineer Samson Luhigo: Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Bandari wakati wa awamu ya 3.

Nawasilisha!!!
 
The Boss kungekuwa na viongozi wengi wa aina ya Masebu kama kweli teuzi zao zingezingatia uwezo na uadilifu wao (meritocracy). Sasa hili alipo kwa kuzingatia utamaduni wa teuzi wa siku hizi katika utawala wa CCM. Vigezo vinavyotumika kwenye teuzi ni uswahiba (cronyism) na kujikomba (sycophancy) na kwa hiyo katika mazingira haya ni vigumu kupata viongozi wanaoonyesha weledi na kujiani. Na kwa mwenendo huu, hatutapiga hatua yoyote kwenda mbele kama taifa!
 
Mkuu The Boss, nikukumbushe vile vile majina ya viongozi wengine waliokuwa wanazingatia sheria, miongozo na kanuni siyo kutekeleza majukumu kwa mihemko na kumuogopa kiongozi wa ngazi ya juu. Wazelendo hawa ni:

(1) Professor G. V. Mmari: Vice Chancellor, Open University, Sokoine University, University of Dar Es Salaam wakati wa awamu ya 2 na ya 3
(2) Engineer Samson Luhigo: Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Bandari wakati wa awamu ya 3.

Nawasilisha!!!


Ahsante kwa kuongeza list..
sasa naona wanayo yaona kwa media yanawaacha mdomo wazi
 
Back
Top Bottom