Harufu ya Uhaya

komedi

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
204
17
HARUFU YA UCHAGA SEASON 2


Mkuu, kama unaikumbuka stori yetu ya harufu ya uchaga....sasa hii ni Part II.

Kinyozi wetu mndengereko baadaye aligundua kuwa mtoto aliyezaa na mchaga anamzidi akili mno akaamua kumfukuza mama na mtoto wake na kisha akaamua kuoa mwanamke wa kihaya ili akizaa mtoto awe na japo harufu ya kihaya akidhani kuwa ingekuwa kwake ni ahueni.

Baada ya muda akafanikiwa kupata mtoto wa kiume na kumwita jina lake Mushaija. Alipofikisha miaka mitano akaanza mchezo ule ule kuweka sh 200 na sh 500 ili achague na mtoto Mushaija hakuchagua chochote na akaondoka.

Safari hii kinyozi wetu akapiga yowe kubwa akidai amezaa taahira. Akaendelea na mchezo huo kwa muda wa miaka 3 bila mafanikio yeyote. Sikumoja aliingia kwake mteja mhaya na akaamua kumweleza stori yote. Yule mteja akamwambia jaribu kumwekea pesa kubwa zaidi.

Siku moja wakati mtoto akiwa na miaka 9 yule kinyozi aliamua kujipanua kibiashara na kuamua kuuza shamba lake ambapo alifanikiwa kupata sh milioni 5. Kabla ya kuzifanyia biashara akaamua amwite mtoto Mushaija akamwekea sh 200 upande mmoja na sh milioni 5 upande mwingine achague. Mtoto Mushaija akacheka sana na hakuchagua kitu akaondoka kabisa nyumbani na jioni yake aliporudi akaomba ruhusa kwa wazazi ili aende Ulaya kusoma.

Kinyozi ''sasa mimi mwanangu nitawezaje kukupeleka ulaya kusoma?''

Mushaija ''Usijali baba nina pesa ya kutosha''

Kinyozi ''kivipi wewe mtoto, usilete balaa humu?''

Mushaija ''Kabla hujauza shamba nilipatana na uliyemuuzia kuwa bei ya mwisho ni shilingi milioni 20 na alishanipa cha juu, nimeweka benki na mambo yote mwanasheria wangu anayaelewa''

Kinyozi akadondoka chini na kuzirai.
 
ha hahaaaaaaaa

uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, mbavu zangu mie!!! jamani nashukuru KOMEDI, kwa kuitengeneza siku yangu ya leo!!!

so tusubiri part III????????
 
Ha ha ha ha ha hi nchi itakua juu kama itaongozwa na mchaga au mhaya lalini sio mndengeleko!!!
 
ha hahaaaaaaaa

uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, mbavu zangu mie!!! jamani nashukuru KOMEDI, kwa kuitengeneza siku yangu ya leo!!!

so tusubiri part III????????

Au kama traveller imeishia season I ikapigwa marufuku. Vinginevyo tutaendelewa kumcheki Mndengereko na mikakati yake.
 
Back
Top Bottom