Mwigulu mjibu Mpina ishu ya Mkataba wa SGR Tabora Kigoma

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Mwigulu Nchemba naona jana umepambana bungeni kumjibu Mpina kuhusu hoja ya Mfumko wa Bei na waliokuelewa wamekuelewa na ambao hawajaelewa hawataelewa.

Kuna jambo kubwa sana Mpina amelizungumzia kuhusu Mkataba wa Kampuni ya China inayojenga reli ya SGR Tabora Kigoma nadhani ni muhimu pia umjibu ili tujue ukweli wa suala hili.

Nanukuu sehemu ya mchango wake kuhusu suala hili.

MKATABA WA TRC NA KAMPUNI YA CCECC YA CHINA

Mheshimiwa Spika
, Mkataba baina ya TRC na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kuhusu ujenzi wa Reli ya SGR kipande cha Tabora-Kigoma (Km 506) kwa gharama ya Tsh. Trilioni 6.34.

Baada ya Mfumo wa TANePS (Tanzanian National e-Procurement System) tarehe 4 Aprili 2022 kuonyesha Mkandarasi Kampuni ya CCECC amepewa zabuni ya ujenzi wa SGR Tabora-Kigoma kwa Tsh Trilioni 6.69 kwa njia ya Single Source, wabunge walitoa tahadhari juu ya uwepo wa dosari za kimanunuzi kwenye mchakato wa manunuzi.

Lakini Serikali ilipuuza tahadhari hiyo na kusaini mkataba huo baina ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya CCECC tarehe 20/12/2022 wa ujenzi wa kipande cha SGR Tabora-Kigoma Kilometa 506 kwa gharama ya Dola za Marekani Bilioni 2.7 sawa na Tsh Trilioni 6.34 na ujenzi huu unatarajiwa kuchukua miezi 42.

Mheshimiwa Spika, Changamoto ya mkataba baina ya TRC na Kampuni ya CCECC ni namna mkandarasi alivyopatikana na gharama za mradi zilivyofikiwa:-

(i) Kutumia njia ya manunuzi ya Single Source kwa mradi mkubwa wa Tsh Trilioni 6.34 badala ya njia ya ushindani inayotoa nafasi ya wazabuni mbalimbali kushindana kwa bei na kwa ubora na kuondoa mianya rushwa na upendeleo kama Sheria na Kanuni zake zinavyotaka.

(ii) Kampuni ya CCECC imeingia mkataba wa Lot Na. 6 Tabora -Kigoma (Km 506) kwa gharama ya Tsh Trilioni 6.34 ikiwa tayari inatekeleza mradi wa Reli ya SGR Lot. Na. 5 kutoka Isaka- Mwanza (Km 341) kwa gharama ya Tsh Trilioni 3.12 ambapo utekelezaji wake ulikuwa 4% tu na kuifanya kampuni hii kupewa jumla ya Kilomita 847 za ujenzi wa SGR kwa gharama Tsh. Trilioni 9.46 kwa wakati mmoja.

(iii) Kampuni ya CCECC haijawahi kujenga hata kipande cha kilomita 1 cha SGR hapa nchini na kukamilika na hivyo sio rahisi kuthibitisha juu ya uwezo na ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya aina hiyo.

(iv) Kipande cha Tabora - Kigoma kimekuwa na gharama kubwa ikilinganishwa na maeneo mengine. Wastani wa gharama ya ujenzi kwa Kilomita 1 ni Tsh bilioni 9.1 kwa miradi ya SGR inayoendelea maeneo mbalimbali nchini (Lot. Na. 5) lakini wastani wa gharama kwa kilomita 1 ni Tsh bilioni 12.5 kwa kipande cha Tabora-Kigoma ambayo ni zaidi ya Bilioni 3.4 ikilinganishwa na maeneo mengine kwa kila kilomita ya SGR. Na hivyo kupelekea malipo yenye mashaka katika mkataba huu kuwa Tsh. Trilioni 1.7
(v) Kabla ya kutangaza Zabuni Serikali ilifanya usanifu na upembuzi yakinifu wa kujenga kipande cha kilomita 514 cha SGR kutoka Tabora-Kigoma kwa gharama ya Tsh Trilioni 4.89 (wastani wa Tsh Bilioni 9.5 kwa kilomita 1 ya SGR) Lakini amekuja kupewa Mkandarasi CCECC kwa gharama ya Tsh Trilioni 6.34 (wastani wa Tsh Bilioni 12.5 kwa kilomita 1 ya SGR) tofauti ya Tsh. Trilioni 1.45 ya usanifu uliofanywa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, njia ya manunuzi ya Single Source iliyotumiwa na Wizara ya Uchukuzi na TRC katika kumpata Mkandarasi CCECC ni ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Manunuzi ya Umma na Kanuni zake za Mwaka 2013 na marekebisho yake ya Mwaka 2016 katika utoaji wa zabuni kwa njia ya zabuni zisizoshindanishwa (single source) ambapo masharti yake yamewekwa katika Kanuni ya 159, 160 na 161.

Mheshimiwa Spika, Njia ya manunuzi ya zabuni zisizoshindanishwa (single source) inatumika kwa mazingira maalum ambayo yamewekwa wazi kwenye kisheria. Manunuzi kwa njia ya Single Source yasipozingatia matakwa ya Sheria yaliyowekwa inaweza kuwa kiini cha rushwa, upendeleo kwa baadhi ya wazabuni, mradi kutekelezwa chini ya kiwango, gharama za mradi kuwa juu kuliko uhalisia, pamoja na kupata wazabuni wenye uwezo mdogo wa kazi.

Mheshimiwa Spika, kuingiwa kwa Mkataba huu kunaleta maswali mengi nini kiliwasukuma Wizara ya Uchukuzi na TRC kukubali kumpata Mkandarasi kwa njia ya Single Source wakati miradi mingine yote ya SGR ilitangazwa kwa uwazi. Lakini pia cha kushangaza zaidi Wizara ya Fedha na PPRA kuruhusu mkataba kusainiwa huku wakijua kuwa taratibu za manunuzi zimekiukwa kwa kiwango kikubwa.

Kwa kuwa, kuna mashaka ya namna mkandarasi alivyopatikana, gharama za mkataba zilivyofikiwa na namna TRC na Wizara ya Uchukuzi walivyojiridhisha juu ya uwezo wa Kampuni CCECC kupewa mkataba wa ujenzi wa Kilomita 847 za SGR kwa wakati mmoja.

Na kwa kuwa, Mamlaka za Usimamizi Wizara ya Fedha na PPRA zimeruhusu Mkataba kusainiwa licha ya kuwepo dalili za ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Manunuzi na Kanuni zake ambao unapelekea kuwepo kwa malipo yenye mashaka ya kiasi cha Tsh. Trilioni 1.7.

Hivyo Basi, Bunge liiagize Serikali kufanya yafuatayo:-

(i) Kuwasilisha bungeni taarifa ya mchakato wa manunuzi kuanzia kutangaza zabuni, tathmini na utoaji wa zabuni ya SGR kipande cha Tabora-Kigoma Kilomita 506 (Kamati ya Miundombinu na Kamati ya Katiba na Sheria zifanye uchambuzi kwa niaba ya Bunge na kuwasilisha taarifa bungeni)

(ii) CAG, TAKUKURU na PPRA wafanye ukaguzi maalum katika mchakato wa manunuzi na kuingia mkataba wa TRC na CCECC wa ujenzi wa SGR kipande cha Tabora-Kigoma Kilomita 506 na taarifa iwasilishwe bungeni ili Bunge liweze kuchukua nafasi yake.
 
Mpina amedhulumu ardhi ekari 1000 huku Morogoro .....ni fisadi wa hali ya juu, kachukua ardhi ya kijiji
 
Shida tunajadili nani kaleta hoja badala ya kujadili alicholeta. Kuhusu ufisadi wake nao uibuliwe mahali panapohusika
Muda mchache mkuu, tunaua ndege wawili kwa Jiwe moja mkuu wangu
 
Waziri wa Ujenzi anafanya kazi gani?

Mpina Huwa ni mkurupukaji
 
Back
Top Bottom