Harufu ya Ufisadi na Ubadhirifu Mkoani Simiyu

Na wewe anzisha SACCOS yako bubu kama wao. Ukikopa songesha vocha ya 500 unarudisha 600 ata ikiwa ni ndani ya lisaa 1 hili unasemaje? Ebu tumsikilize mkurugenzi yeye anasemaje?
 
Hali ya Watumishi wa Umma wilayani Maswa ni mbaya sana kwani Watumishi wa kada za elimu na afya wanalazimishwa kukopeshwa fedha nakwa kupitia Saccos bubu iliyopo ndani ya Halmashauri(Inayo milikiwa na Mkurugenzi pamoja na baadhi ya Maafisa utumishi) kwa riba ya asimilia 20 kwa mwezi.

Ndani ya Halmashauri ya Maswa Dc Viongozi wa Halmashauri husika wamekuwa na Tabia ya kujichukulia sheria mkononi kama vile wao ni mahakama.Hii imepelekea watumishi kuwa waoga hata kudai haki zao za msingi,kwa kuhofia mkono wa chuma wa viongozi wa Halmashauri Maswa Dc.

Ajabu ni kwamba watumishi wa umma waliopo ndani ya Halmashauri hii hasa kada ya Elimu na Afya hawana Furaha ya kutumika ndani ya Halmashauri hii,Walimu na wahudumu wa afya wamelazimishwa kuchangia Shilingi 5,000/=kila mmoja toka kwenye mshahara wake(makato ya Moja kwa moja?ili kuchangia shughuli za mbio za Mwenge.

Je,ni kwamba Serikali haina bajeti husika kuhusu mwenge?Kwanini tuwapokonye hata hiki kidogo walichonacho hawa watu ambacho wanajipatia kwa taabu.

Waziri wa Tamisemi na Mkuu wa mkoa wa Simiyu mnapaswa kujua hili na kama mnalijua basi mlichukulie hatua haraka iwezekanavyo,huu ni unyanyasaji wa kiwango cha hali ya juu zaidi kwa watumishi hawa ambao baada ya miaka mitano tunawaomba watuchague tena tukiwachukulia kama kundi muhimu sana.

Jambo lingine mpaka sasa tangu Waajiriwa wapya wa kada za afya na elimu waripoti kazini 28/07/2022 Mapaka leo hawajaingiziwa hata shilingi kumi kwenye akaunti zao hata pesa ya kujikimu,Je bado tutarajie uzalendo na huduma bora toka kwa Watumishi hawa?

Mtu aliyepelekwa eneo kama Ikungulyankhoma anaishije ilihali hana hata pa kuanzia na ni mwezi sasa umepita.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu ameanzisha Saccos bubu ndani ya Halmashauri ambapo wanawakopesha Watumishi wapya fedha za kujikimu kwa riba ya Asilimia 20 kwa mwezi.



Je hii SIMIYU (Maswa) ni nje ya Tanzania?
Kiongozi poleni sana, kuna wilaya maafisa utumishi wezembe sana. Wakati kuna wilaya ajira mpya washaanza kupata mishahara kuna zingine mnaweza kusubiri hata miezi mitatu, pesa ya kujikimu nayo uchelewa hata miezi 2
 
Mbona kama unalimnda mkurugenzi?
Ni muhalifu kama wahalifu wengine yule jamaa, huwezi anzisha Saccos bubu kisha uwakopeshe watumishi ambao hujawalipa mishahara halafu uwe ni msafi.
Wewe mleta Mada ni Mfitini na Mtu ambaye aidha ni mjuaji usiye na akili kichwani. Hao watumishi unaosema wameripoti tarehe 28/7/2022 at the same time unasema hawajapewa mshahara wala posho. Huo mwaka ni wa kalenda ya Nchi gani???
Unalalamikia makato ya elfu 5?? Kisa Mwenge??? Unajua maaana ya Team work Building??? Hujui kwamba wakati wa Mwenge ndio Tamasha pekee watumishi hukutanishwa kucheza, kunywa na kula pamoja?? Sasa wewe unataka mbinu za Kiuongozi za DED zifanane na Mtizamo wako?
Kama wewe ni ajira mpya punguza kiherehere Utumishi wa Umma hauko hivyo!
Eti SACCOS unaona haifai?? Ulitaka watumishi waende Bayport au Maboto ambako riba ni 40%???
Anyway watu wa dizaini yako ni wachawi ambao mmekosa zana lkn moyoni wewe ni mchawi sana.
 
Back
Top Bottom