Wiyelelee
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 1,071
- 348
Umewahi kukutana na mtu mwenye harufu mbaya ya kikwapa? Mwaka jana, nilikuwa ofsini nafanya kazi kama kawa mida ya ashubuhi. Pembeni kulikuwa na chai yangu. Aliingia dada mmoja hivi, du! Hata hamu ya kunywa chai iliishia hapo. Japo alihitaji ushauri wa kitalaam, nilimvumilia sana na nilipomalizana nae, ilinibidi nifungue madirisha yote ili harufu mbaya itoke. Alikuwa na harufu ya kikwapa ile mbaya, japo alivaa vizuri sana na ni mrembo.
Jana tu nilikuwa na mkutano kwenye ofisi moja kubwa. Jamaa niliekaa nae karibu balaa! Sijui aliweka mzoga wa panya kwenye kikwapa ata sielewi. Nilipomtazama vizuri, nikakuta ana pete ya ndoa! Nikajiuliza hivi mke wake hasikii harufu hiyo? Jamani, huenda huyu mtu anasoma JF hapa, hebu msaidie aondokane na harufu ya kikwapa. Mezani tuliwekewa juice ya azam na korosho wala sikugusa kitu, hata maji sikunywa kabisa.
Wewe mke wa huyu jamaa, huoni aibu? Au na wewe una tatizo la kikwapa? Watu wengine bwana...