Harmorapa akiri kwenda kwa mganga wa kienyeji kisa penzi la Wema Sepetu

Joram Dymisster

JF-Expert Member
Apr 7, 2014
502
418
1.jpg


Msanii wa muziki wa bongo fleva Harmorapa amefunguka na kusema kuwa katika mwaka 2017 amehangaika kulipata penzi la mwanadada Wema Sepetu kiasi cha kuamua kwenda kwa mganga wa kienyeji mara tatu ili aweze kumpata mrembo huyo.

Harmorapa akiongea kwenye kipindi cha eNewz cha EATV amedai kuwa baada ya kuhangaika kwa marafiki zake Wema Sepetu na kugonga mwamba aliamua kwenda kwa babu (mganga) ambapo amedai kwa mara ya kwanza aliambiwa apeleke kuku mweupe, na alipeleka huyo kuku lakini aliporudi mjini Dar es Salaam mambo yake yakawa bado vile vile.

"Nimemuendea kwa babu Wema Sepetu mara tatu, nilipokwenda mara ya kwanza niliambiwa nipeleke kuku mweupe, nikapeleka zangu yule kuku mganga akafanya yake lakini niliporudi mjini sikuona mabadiliko yoyote yale, nikamfuata tena babu akaniambia nipeleke vitu vingine viwili ambavyo hapa nashindwa kuvisema" alisema Harmorapa

Harmorapa aliendelea kufunguka jinsi ambavyo amehangaika kulitafuta penzi la Wema Sepetu na kudai ilifika wakati aliambiwa apeleke mchanga wa unyayo wa Wema Sepetu au mchanga ambao mwanadada huyo ametemea mate, kitu ambacho Harmorapa amedai kilikuwa kigumu sana kwake kwa sababu hapati nafasi ya kukutana live na Wema Sepetu.

Hata hivyo Harmorapa kwa sasa amesema amemwachia Mungu juu ya jambo hilo baada ya kuona harakati za kwa mganga wa kienyeji zinakwama.
 
Nilimuona hata Mimi, kwanza hajiamini akiwa anaongea, ni mpuuzi kabisa na sijui kwanini kumpa platform kijana ambaye hata producer MJ hajawai mfahamu halafu anajiita naye ni msanii...
 
Huyu naye mzigo kwelikweli, kukimbilia njia za mkato.

Si akazane kwenye hiyo sanaa/mziki wake awe kama Diamond aone huyo Wema atapenyea wapi?
 
Back
Top Bottom