Harmonize atakuwa msanii wa kwanza kujitenga WCB

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
3,317
2,000
Harmonize....Sitaaki Kuongelea Zile Haso zake za BSS....zile haso zake za kutoka hadi Diamond kuja kumuona Na kuamua Kumsign Na kuwa msanii wake Chini ya WCB! Alitoa Aiyola ikamtambulisha....akaachia Kidonda changu ikamuongezea utambulisho lakini Diamond Alimtambulisha zaidi na Zaidi kupitia show na Kuamua Kushi nae Nyumba Moja! Mwishowe akumueka kwenye nyumba Yake alionunua Diamond! Ila sahizi sijui Wapi anakaa.....Bado ikamzidisha kumtambulisha hadi sasa pamoja na Kiki zote!

Mimi shabiki wa WCB na Nina wapenda wasanii pale....lakini Kasumba Moja kubwa ya wasanii wa WCB ni hawajui kufanya INTERVIEW....hilo liko wazi na Hapo ndipo huwa wanafeli japo majigambo kwa Msanii ni kawaida!

Ila Harmonize hajui INTERVIEW kuliko msanii yeyote pale WCB kujieleza hajui ni mtu anae tamani kuongea kila kitu kwenye Interview Moja! Pamoja na Tabia zake zingine Lakini sijui

Ila naweza kusema kuwa HARMONIZE atakuwa msanii wa kwanza kujitenga na WCB na hata ondoka kwa Mazuri watagombana sana Kupitia Media na huo utakuwa mwisho wa HARMONIZE ......Kama huamini haya niyasemayo Jaribu kufuatilia interview zote za HARMONIZE hivi karibuni utaelewa nacho ongea......Managament yake na Harmonize hamna dalili nzuri siwezi sema ni Kisa MZUNGU ila Harmonize anatabia fulani hivi si nzuri japo sijaishi nae!.....Harmonize nilicho jifunza ana Nidhamu ya woga na hii itamfanya asepe Mapema WCB

Dalili ya Mvua ni Mawingu.....Wazungu wasema Time Will Tell....Ngoja nitunze akiba ya Maneno yangu lakini akili yangu inanituma na kunambia kuwa HARMONIZE atakuwa msanii wa kwanza kujitenga WCB na watagombana na Kundi la WCB

Ingekuwa ni uwezo wangu ningezuia hiki kisitokee lakini sina jinsi mm ni mshabiki wa kawaida tuu!!! Ila yule MZUNGU SIJUI kama WCB wamemkubali nafikiri hapana......Japo HARMONIZE KUWA na MZUNGU mimi sio sababu ya Kusema Kuwa HARMONIZE ATAJIENGUA WCB!

Ila kwa Dalili hizi......mmmmmmh

Danya
 

The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
7,665
2,000
Dogo ana bidii ya kazi Sana, kwani kutoka WCB kitu gani bwana.... prof Jay alikuwaga Hard blasters ujue
Sasa prof jay wa hard blasters si ndo kama diamond wa WCB, wako wapi akina terry na fanani?

Amin diamond ni diamond na atakuwepo hapo ila hawa wasanii wake hawatafika popote, labda mmoja au wawili, ukiangalia foundation ya platnumz ni hatari, na mkiomba njaa ndo kwanza anavuna sema uswahili tuu kukulia tandale ni shida
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom