Harmonize atakuwa msanii wa kwanza kujitenga WCB

Sasa prof jay wa hard blasters si ndo kama diamond wa WCB, wako wapi akina terry na fanani?

Amin diamond ni diamond na atakuwepo hapo ila hawa wasanii wake hawatafika popote, labda mmoja au wawili, ukiangalia foundation ya platnumz ni hatari, na mkiomba njaa ndo kwanza anavuna sema uswahili tuu kukulia tandale ni shida
Najua hilo , wote nawaona kama wapo level moja hivi, tofauti ni kwamba mmoja alimtangulia mwenzake......

Kama unakumbuka enzi za kina Pack na Big...... Waliofaidi ni kina Jigger na Diddy..... It's about time....... Sema kukulia uswahilini bila exposure na Training on public speaking madogo wote hata Mondi watazingua Sana......

Anyways.....nawaombea sana kina Aslay
 
Hebu tupe mfano Wa neno aliloongea linaloweza kumletea shida shida kubwa nimemuona nayo ni kumuiga diamond 200% kuongea ktkt interview mpaka swaga..za kuongea mpangilio Wa maneno kucheka loo uunaweza kudhani anayehojiwa ndiye dangote mwenyewe hapo tu ila sijaon shida zaidi ya nidhamu ya hali ya juu
 
Acheni wivu
Mkuu sina Wivu na Harmonize kwa sababu..Kufanikiwa kwakwe au kutokufanikiwa kwake Hakuna Impact yoyote kwangu...Pili yeye ni msanii na mm nina kazi nyingine tofauti kabisaa na Usanii nimuone wivu wanini? Yeye ana Mpenzi wake mzungu mimi wangu muafrika wivu wa nini? Anaishi Dar mimi naishi mkoani huko nitamuoneaje wivu
 
Sio kaongea na Shilawadu hiyo Interview sijaifuatilia ila Harmonize Interview nyingi hawezi kujieleza....Alifanya interview na XXL sikumuelewa Meneja anasema hiki na yeye anasema hiki
Unachosema kuhusu interviews nakubaliana na wewe, Harmonize anashindwa kujua ni Mambo gani ayazungumzie na mambo gani amwachie Manager ( eg kuwa wa kwanza kutangaza Rich Mavoko kasainiwa WCB kabla ya muda ).Hapa naona Rayvanny anamzidi ingawa kila mtu ana matatizo yake( Kukataa kumzungumzia Qboy kwamba uongozi ndio wenye majibu. Ila mimi binafsi sishangai kwasababu Wabongo tuna utamaduni wa kulazimisha kuzungumzia kila kitu hata kama hatukijui vizuri, na ishtoshe Harmonize huwa anakuwa escorted na Ricardo Momo ambaye hajui chochote kuhusu management na mwoga wa kuongea kwenye media. Anyway nadhani tatizo lake ni dogo na linarekebishika ni maamuzi yake tu
 
Katika kundi lao WCB yoote hakuna msanii anaejua kuimba vizuri kama Harmonize nakuambien Harmonize hata akiondoka wasafi atagombaniwa na menegmnt kibao hapa bongo na nje ya Tanzania ana nyimbo zenye maisha marefu sana mfano Aiyola Bado Hbd Niambie ni nyimbo zinazoishi milele kwa tungo sauti na melody laini ya kubembeleza ila Huyo Lava lava ndio kashaisha Raymond atabaki tu kwa sababu ni mtoto wa marehemu chande yaan tangu aanze ana nyimbo moja tu KWETU zingine zinakuja lakini hazina ujumbe wala ladha wala nin yaan Kimziki Raymond ni wakawaida sana kama sio promo hana heat song. Mavoco sina neno lakini hajafit kwenye ala za WCB nadhani ana anga zake sio pale ni hayo tu lingine sina.
 
Ofkoz mzungu tunasikia ana pesa au mihela ya kutisha sasa abakie huko wcb kufanya nini na hizo pesa ndo zimenzidishia kiburi saivi kama ka change hivi anyway ni maisha yake
 
Jamani interview ni kitu kigumu sana unaweza kuwa msomi usijue kuhojiwa ni kama hotuba huwa zina wenyewe. Kwa hapa bongo msanii anayejua interview ni Omy dimpoz tu wengine wanaunga tu. hawajui chochote yaan bora wamejibu swali tu yaan Dimpoz akimaliza interview husikii gazeti likiendeleza interview wala udaku kinachobaki ni chuki wivu na pongezi tu kwa dimpoz sio siri huwa anaua kabisa
 
Back
Top Bottom