MSIMISEKI SENIOR
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 459
- 287
Nimejaribu kufikiri kuhusu huyu mtu anayeitwa HARBINDER SINGH SETH ambaye amekuwa gumzo kubwa nchini kufuatia kashfa ya uchotwaji fedha kwenye akaunti maalum inayofahamika kama ESCROW ACCOUNT iliyokuwa imefunguliwa kwa pamoja kati ya TANESCO na IPTL kupitia B.O.T
Jambo kubwa lililonifanya nijiulize maswali mengi ni baada ya kusikia taarifa za uhusika wa SETH katika kashfa nyingine inayofanana kwa karibu na hii ya ESCROW ambayo ilitokea nchini kenya maarufu kama ''GOLDENBERG SCANDAL'' ambayo bwana SETH pia alihusika akiwa miongoni mwa watuhumiwa wengine 12.
Kwa mujibu wa mtandao wa WILIKEAKS: https://wikileaks.org/wiki/KTM_report#Harbinder_Singh_Sethi Seth inaonekana ni raia wa KENYA mwenye asili ya ASIA mbaye alikimbilia/alihamia Afrika Kusini mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa KENYA mwaka 1997. Pia, kwa mujibu wa wkileaks SETH alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya rais wa wakati huo ARAP MOI ambaye kwa kumbukumbu alihusishwa na kashfa ya GOLDENBERG ambayo kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya siasa ndiyo iliyopelekea chama tawala wakati huo KANU kuanguka vibaya ktk uchaguzi mkuu.
Ukisoma kwa kina taarifa ya WIKILEAKS kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika UINGEREZA (U.K) Seth aliwahi kumiliki kampuni 3 kama zinavyonukuliwa hapo chini;
Ukisoma taarifa zaidi zinaonesha katika kashfa ya GOLDENBERG Seth alihusika moja kwa moja na utakatishaji wa fedha zilizochotwa kupitia baadhi ya bank huko KENYA kwa kushirikiana na baadhi ya Bank nyingine duniani.
Hivi wakati yote haya yanatokea kwa jirani zetu KENYA ni kweli serikali yetu haikulifahamu hili? je haikufahamu uhusika wa bwana H. SETH katika sakata la GOLDENBERG hadi wafikie uamuzi wa kuingia naye mikataba kupitia kampuni zake za mfukoni ambazo mwisho wa siku zinaliacha taifa katika hali tete?
Hapa swali la msingi, je Serikali wakati inatafuta wabia wa kufanya nao miradi mikubwa huwa inatumia vyombo vyake na taasisi zake ipasavyo kufanya uchunguzi wa kina juu ya taarifa sahihi za wabia wake? au kwa sababu mbalimbali zikiwemo 10% mambo huachwa yaende tu huku kukiwa na kinga ya wakubwa? je hali hii inayoliingiza taifa hasara mara kwa mara umekuwa mradi endelevu wakati WATANZANIA wakizidi kuteseka huku maisha yakizidi kuwa magumu? kwa taarifa iliyotolewa bungeni wakati wa mjadala wa ESCROW imetamkwa kwamba TANESCO kila mwaka inazidi kupata hasara na zote zinatokana na mikataba mibovu hasa IPTL wakati huo huo waziri Prof Mhongo anasisitiza kushusha bei ya umeme kitu ambacho siyo cha kweli kwani sasa hivi umeme upo juu kuliko yanayosemwa.
Ni wakati umefika sasa WATANZANIA tujifunze. Pamoja na kuwataka viongozi kuwajibika lakini mimi binafsi bado nalilia mfumo tulionao ambao ndiyo chanzo cha matatizo yote.
MUNGU IBARIKI NCHI YANGU TANZANIA(TANGANYIKA)

- Canray Ltd, a company currently in liquidation from which he resigned in 1998
- Basic stone Ltd, a dissolved company from which he resigned in 1995
- Hollywood Electronics Ltd, a dissolved company from which he resigned in 1993