Harbinder Singh Sethi aliyenunua IPTL ni nani?

Harbinder Singh Sethi aliyenunua IPTL ni nani?

Wizara ya Nishati na Madini sijui awekwe nani pale ili angalau watanzania wapumue... Godwin Ngwilimi mwanasheria wa TANESCO amejiuzulu? Tafadhali mwenye data atumwagie hapa jamvini...
 
Wapi TISS wetu jamani? Issue kama hizi zilikuwa wawe wamesema lolote. Au kazi yao ni kudeal na kina chadema, madaktari na walimu tu? Mara meno ya tembo na sasa wameingia hadi BoT kwa mara ya pili bado wao wamepiga kimya tu! Wapi uzalendo wao kwa wanaowalipa mshahara? Hebu watuonee huruma sisi tunaojichangisha vikodi vyetu kuwalisha na kuitunisha hazina yetu. Na huu mtindo wa familia za watawala kukimbilia kwenye kihenge kujichotea tuuu ni kitu gani? Hii ni aibu kiukweli hata mkituchekea mhmh! Hapana. Wawajibishwe wote bila kuangalia sura.
 
Nasikia Joseph Mungai ni Mkenya alietekeleza madeal mengi chini ya utawala wa CCM!

Ni kweli baba yake ni mkikuyu; huyu Mungai alitumia ubunge wa Mufindi kuhodhi maeneo makubwa ya ardhi wilayani Mufindi, ni fisadi wa kutupa!!!
 
Huyo singa singa ni wanted nhi kibao ikiwemo Kenya lo sie ndio tunamuona muwekezji?
 
Prof.Muhongo kaingia king!alete tena madharau yake.hii wizara ni ngumu sana
 
Mkuu kiongozi ni mtawala mwenye kufuata maadili ya kazi kwenye utawala yaani Ethical Leadership is leading by knowing and doing what is right... Kama hafuati misingi hiyo huyo ni mtawala tu. Nadhani Africa tuna uhaba wa Viongozi ama hawapo kabisa baada ya wale wachache tuliopewa kwa majaribio ( Kwame Nkurumah,Nyerere,Mandela,Machel, Naser....) kumaliza incubation period yao duniani kwenye kufanya feasibility study!
Mkuu nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa sana LAKINI usisahau kuwa mabeberu wako makini, wana mafungu ya kutosha kupindua serikali yoyote ile ktk Africa! Suala la kuhujumiwa kwa TANESCO kwa nyakati tofauti na hata kuwaleta netgroup solution ilikuwa ni ku-pave ways kwa Exxon Mobil via Symbion kuja kuchukua kazi zote za TANESCO! Wao wanajua kuwa waki-control power wanakuwa wame-control uchumi wa nchi hivyo kutufanya kuwa tegemezi wa bidhaa kutoka nje! Tambua kuwa makampuni mengi ya kimarekani yalipeleka uzalishaji China na sasa wanatafuta masoko kila kona ya dunia hii... Wachache tunajua kuwa Sysmbion soon wataanza uzalishaji na wateja wao wakuu ni migodi na viwanda vichache ..TANESCO watabakia na wateja wa majumbani ambao hawalipi kodi plus vishoka kila kona ... we are done Mkuu...my be next generation wanaweza kufanya vizuri zaidi...
 
huyo profesa wa nishati aje kuongea mbovu kama alivyozoea sasa
 
Moja ya hadidu za rejea ni uchunguzi wa iwapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) aliisamehe kampuni hiyo kodi inayofikia Sh26 bilioni.

What I know hawa jamaa walilipa kodi bilioni 32 labda kama kodi ilipaswa kuwa bilioni 58.
 
The Rostam's


images


Mr Harbinder Singh Seth akitoa Shs11,000,000 kwa George Kashushura, Kiongozi wa SACCOSS ya Kanisa la MT RITTA KIMARA DSM .Pesa hiyo imetolewa tarehe 21/3/2014 siku chache baada ya kukwapua fedha BOT

Hapo yupo na mwanasheria wa PAP aitwaye JOSEPH MAKANDEGE ambaye ndiye amemuunganisha Singa Singa (tapeli ) na Makanisa.Hata hivyo zipo taarifa kuwa Albert Marwan a Singa Singa huyo ni pete na kidole !!

 
Back
Top Bottom