Harambee na michango nyumba za ibada zimeishia wapi?

Harambee na michango nyumba za ibada zimeishia wapi?

23 March 2015 Mtatiro aliwahi kutamka haya maneno yanayohusiana na picha hii

NJAA HADI KWENYE NYUMBA ZA IBADA!!!!

Askofu.jpg

Wachungaji wa makanisa mbalimbali ya Kikristo wakiandamana muda huu kwenda nyumbani kwa Edward Lowassa kumshinikiza achukue fomu ya kugombea Urais.

I hope mapadre hawamo humo! Mungu atuepushie!

Yani kanchi ketu haka kanaendeshwa kwa ujanja ujanja na wiziwizi tu. Mtu akiwa na hela zake basi anafanya jambo lolote tu, Duh!

Julius S. Mtatiro (23 march 2015) (FB page)

My take:
Akiba ya maneno ni muhimu ( Shetani wa jana hawezi kuwa malaika leo)
 
Kwani nini hakiko sawa?

Ukweli wa hayo maneno ndo yamedhihirishwa

Nchi inaendeshwa kwa ujanja ujanja na wiziwizi tu.

Mtu akiwa na hela zake anafanya jambo lolote.

CCM ndo imetufikisha huko kwa mfumo wa utawala ambao kigogo wa chama ndiye bosi wa kila kitu ndiye mwenye maamuzi ya kila kitu sera za nchi na mipango inapangwa na watu wachache wenye pesa zao wanaoiba mali ya nchi.

Mwenye pesa ndiyo mwenye nchi.

Tunashuhudia ufisadi wa kiwango cha kishetani watu hawaguswi.
 
Kabla ya kuandika kitu chochote ambacho utakishare kwa jamii ni vema ukawa na utulivu wa akili,,hebu tuambie ni nchi ipi duniani ambayo matajiri hawana nafasi ktk utunzi wa sera za nchi yao? wewe kama uchumi wa kaya yako umeshindwa kuendesha ukatengemaa bado wataka uwe na nafasi ya kutufundisha? mada imeeleza undumila kuwili wa wanasiasa wetu wa upinzani ikinukuu matamshi ya Mtatiro,,wewe unakimbilia kusema ccm ndo imekufikisha hapa kwani ccm wamekushikia akili? Kwahio ccm wakisema upewe bwana utakubali kwakua ndo imekufikisha hapo? Wenye pesa lazima wawe na nafasi tu kwani ndo walipa kodi wakubwa wewe subiri serikali ikusanye kodi kwa wenye nazo wewe usomeshewe watoto wako bure maana ukishakua masikini kazi yako ni kuzaa tu.
 
Kwani nini hakiko sawa?

Ukweli wa hayo maneno ndo yamedhihirishwa

Nchi inaendeshwa kwa ujanja ujanja na wiziwizi tu.

Mtu akiwa na hela zake anafanya jambo lolote.

CCM ndo imetufikisha huko kwa mfumo wa utawala ambao kigogo wa chama ndiye bosi wa kila kitu ndiye mwenye maamuzi ya kila kitu sera za nchi na mipango inapangwa na watu wachache wenye pesa zao wanaoiba mali ya nchi.

Mwenye pesa ndiyo mwenye nchi.

Tunashuhudia ufisadi wa kiwango cha kishetani watu hawaguswi.
Kwa CCM ni mafisadi.Kwingineko wakihamia ni WATAKATIFU!.
 
Kwani nini hakiko sawa?

Ukweli wa hayo maneno ndo yamedhihirishwa

Nchi inaendeshwa kwa ujanja ujanja na wiziwizi tu.

Mtu akiwa na hela zake anafanya jambo lolote.

CCM ndo imetufikisha huko kwa mfumo wa utawala ambao kigogo wa chama ndiye bosi wa kila kitu ndiye mwenye maamuzi ya kila kitu sera za nchi na mipango inapangwa na watu wachache wenye pesa zao wanaoiba mali ya nchi.

Mwenye pesa ndiyo mwenye nchi.

Tunashuhudia ufisadi wa kiwango cha kishetani watu hawaguswi.
Lofa ktk ubora wake!
 
pia mtatiro alipo lindwa na polisi ili aingie ofisi kwakwe aliwasifu na kusema ni haki yake kupata ulinzi kutoka kwa polisi.
lakini walipo mlinda lipumba alisema polisi wanatumika
 
23 March 2015 Mtatiro aliwahi kutamka haya maneno yanayohusiana na picha hii

NJAA HADI KWENYE NYUMBA ZA IBADA!!!!

View attachment 416054

Wachungaji wa makanisa mbalimbali ya Kikristo wakiandamana muda huu kwenda nyumbani kwa Edward Lowassa kumshinikiza achukue fomu ya kugombea Urais.

I hope mapadre hawamo humo! Mungu atuepushie!

Yani kanchi ketu haka kanaendeshwa kwa ujanja ujanja na wiziwizi tu. Mtu akiwa na hela zake basi anafanya jambo lolote tu, Duh!

Julius S. Mtatiro (23 march 2015) (FB page)

My take:
Akiba ya maneno ni muhimu ( Shetani wa jana hawezi kuwa malaika leo)
Kwa wale wa imani ya Kikristo fumbo hili la Lowassa na Lipumba mbona linapata tafsiri sahihi kutoka katika maandiko juu ya Yuda na Sauli (Paulo).
Yuda alikuwa mwanafunzi mwaminifu wa Yesu na mmoja wa wale tenashara (12) na kwa jinsi alivyokuwa anapendwa mpaka alikuwa anakaa miguuni pa Yesu kwa kipindi chote cha Yesu kueneza injili. Lakini mwishoni kabisa alipokea hongo na kumsaliti Yesu na mpaka Leo ni adui mkubwa kwa wakristo na mfano mbaya.
Lakini Sauli aliogopwa sana kwani alikuwa anawaua viongozi na wakristo wa zama hizo, alifanya hayo bila woga na wapinga ukristo walimtumia kutimiza dhamira zao. Baadae alitokewa navkubadilika kisha akaitwa mtume Paulo. Paulo anaheshimika sana ndani ya ukristo na ni mtu mjinga tuu ndiye anaweza kusema mbona alikuwa mbaya kwa nini sasa Paulo asafishwe na kusikilizwa?
Yuda=Lipumba (amevunja uaminifu wake)
Sauli=Lowassa (amejua alikosea wapi ameongoka na kuijua kweli kama mtume Paulo alivyofanya).
Hivyo kwa mwanadamu anayesema Lowassa hawezi kubadilika na kuaminika basi hana sababu ya kumwamini mtume Paulo kwani huyo alikuwa mwizi, katili na muuaji kabisa.
 
  • ACHANGISHA MILIONI 103/-,AMMWAGIA SIFA MKAPA
Na Mwandishi Wetu, Masasi

W
aziri Mkuu aliyejiuzulu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa, amesema yuko tayari kushirikiana na mtu yeyote katika mapambano ya kuondoa umaskini kwenye jamii.

Bw. Lowassa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Mjini Masasi mkoani Mtwara, katika harambee iliyofanyika kwenye Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Masasi, mkoani humo.
Harambee hiyo ilikuwa na lengo la kuchangia shughuli za maendeleo za Ushirika wa Mama wa Kikristo (UMAKI) na kusisitiza kuwa, yeye ni mdau wa mapambano hayo.

“Mtu yeyote anayepambana kuondoa umaskini katika jamii, niko tayari kushirikiana naye katika harambee za harakati hizi,” alisema Bw. Lowassa na kuongeza kuwa, wanawake ni jamii inayochukia sana suala zima la umaskini.

“Wanawake ni wadau wakubwa wa kupambana na umaskini ndiyo maana chama changu CCM, katika rasimu ya Katiba Mpya inataka kuwe na asilimia 50 kwa 50 ya uwakilishi bungeni kati ya wanawake na wanaume kwa sababu kinawapenda,” alisema.

Alisema kwa sababu hiyo, ndiyo maana ameridhia kushiriki harambee hiyo ambapo kufika kwake kanisani hapo kumetokana na Wilaya hiyo kutoa kiongozi makini, mwadilifu na shupavu mkubwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa.

“Hapa pana historia ya kutoa kiongozi aliyeiongoza nchi yetu kwa uadilifu na umakini mkubwa, walikuwepo watu waliyojaribu kumsema sema katika vyombo vya habari.
“Mwisho wa siku watu hao wamekiri kuwa Bw. Mkapa alikuwa kiongozio makini,” alisema Bw.

Lowassa ambaye wakati kiongozi huyo akiwa madarakani, alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano kabla ya kupelekwa Wizara ya Maji na Mifugo.
Katika harambee hiyo, zaidi ya sh. milioni 103 zilipatikana ambapo Bw. Lowassa na marafiki zake alichangia sh. milioni 10 na kuvuka lengo ambalo lilikuwa sh. milioni 100.

Chanzo Majira
03 December 2013

Swali langu, amabalo najiuliza imekuwaje Lowassa na marafiki zake hawaendelei kuchangisha na kama ilivyokuwa ada yao hapo awali au issue ilikuwa ni urais 2015? ASANTE MUUMBA, KWA KUTULETEA MAGU, sijui wangelipana nini kurudisha fedha zao walizochangisahana kha, kweli Mungu anajua tusiyoyajua yaliyomo katika vifua vya waja wake.
 
Back
Top Bottom