Harakati za kuondoa ObamaCare zaanza Marekani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Wabunge wa Congress nchini Marekani, ambao wengi wanawakilisha chama cha Republican, wamepiga kura ya kuanza kubadilisha sheria ya Bima ya afya inayofahamika kama Obama care iliozinduliwa na rais Barrack Obama

Bunge la seneti pia limepitisha kura hiyo, ambayo inahitaji kamati za bunge kuanza kuandika upya sheria hiyo.

Hata hivyo baadhi ya wabunge wameonekana kupinga kura hiyo, wakisema ni lazima kuwe na sheria mbadala, kabla ya kufuta ObamaCare.

Hata hivyo bwana Trump anayetarajiwa kuchukua hatamu za uongozi wiki ijayo, amesifu wabunge hao, na akaandika kwenye Twitter, 'ObamaCare itazikwa kwenye kaburi la sahau hivi karibuni.

Chanzo: BBC
 
Hicho ndo trump raisi wa dunia, alisema ataanza nacho, anasisitiza atafuta vitu vyote alivofanya kiongozi dhaifu katika historia ya america(obama).
 
Wabunge wa Congress nchini Marekani, ambao wengi wanawakilisha chama cha Republican, wamepiga kura ya kuanza kubadilisha sheria ya Bima ya afya inayofahamika kama Obama care iliozinduliwa na rais Barrack Obama

Bunge la seneti pia limepitisha kura hiyo, ambayo inahitaji kamati za bunge kuanza kuandika upya sheria hiyo.

Hata hivyo baadhi ya wabunge wameonekana kupinga kura hiyo, wakisema ni lazima kuwe na sheria mbadala, kabla ya kufuta ObamaCare.

Hata hivyo bwana Trump anayetarajiwa kuchukua hatamu za uongozi wiki ijayo, amesifu wabunge hao, na akaandika kwenye Twitter, 'ObamaCare itazikwa kwenye kaburi la sahau hivi karibuni.

Chanzo: BBC
Ni rahisi kusema kuliko kutenda. Mwanzoni alisema ataifuta kabisa, juzi alisema ataibadilisha sasa hivi anasema atafanya vyote viwili kwa mara moja. Ukiwa nje ya uwanja ni rahisi kukosoa lakini ukiingia uwanjani miguu inaanza kuwa mizito. Ni dhahiri kuwa kuifuta "Obamacare" bila mubadala haiwezekani. Na mubadala wa "Obamacare" republicans (GOP) hawana. Siasa ni mchezo ambao hauitaji hasira.
 
Utasemaje haiwezekani wakati hatua zimeshaanza kuchukuliwa kwenye congress na senate? Wao wanachohitaji ni kuifuta na walishajaribu kufanya Mara 60 bila ya mafanikio sababu ya upungufu wa namba yao., maswala ya mbadala wala si kati ya mahitaji yao, hivyo by the time being wataendelea na utaratibu wa zamani kabla ya hiyo Care Act ya Sasa.
 
Wabunge wa Congress nchini Marekani, ambao wengi wanawakilisha chama cha Republican, wamepiga kura ya kuanza kubadilisha sheria ya Bima ya afya inayofahamika kama Obama care iliozinduliwa na rais Barrack Obama

Bunge la seneti pia limepitisha kura hiyo, ambayo inahitaji kamati za bunge kuanza kuandika upya sheria hiyo.

Hata hivyo baadhi ya wabunge wameonekana kupinga kura hiyo, wakisema ni lazima kuwe na sheria mbadala, kabla ya kufuta ObamaCare.

Hata hivyo bwana Trump anayetarajiwa kuchukua hatamu za uongozi wiki ijayo, amesifu wabunge hao, na akaandika kwenye Twitter, 'ObamaCare itazikwa kwenye kaburi la sahau hivi karibuni.

Chanzo: BBC
Safiii
 
Alisema "Care Act" siyo 'Obama Care'
Affordable Care Act ndiyo ilipewa na jina na Republicans wakaiita Obamacare ili kuiroga na kuifanya inuke hasa miongoni mwa wale ambao hawajui maana. Imedhihirika hivi karibuni kwamba wengi waliompigia Trump hawakulijua hilo.
This Man Celebrating The End Of Obamacare On FB Didn’t Realize He Was Actually On Obamacare

Hofu sasa imeshaanza kutanda sasa kwamba bima waliyokuwa nayo ndiyo inayeyuka kutokana na uchaguzi walioufanya.

After Voting For Trump, Coal Miners Terrified To Lose Obamacare
 
Back
Top Bottom