Haraka haraka haina baraka! Subira yavuta kheri

Juzi niliingia hotelini nikiwa na njaa kweli na baada ya kupitia menyu, niliagiza chakula.
Baada ya kama dakika 20 kundi la vijana wa kike na wa kiume waliingia na kuagiza chakula pia. Kwa mshangao wangu, watu hawa walihudumiwa kwanza kabla yangu. Niliwatazama walivyoanza kula na kucheka kimoyomoyo. Na nilimsikia mmoja wao akijigamba jinsi alivyo na uhusiano na kila mtu katika hoteli hiyo na nilihisi kudhihakiwa sana.

Niliamua kuondoka. Sikuweza kuvumilia tena, lakini mhudumu alinifuata na kuniambia kwa utulivu: "chakula chako ni oda maalum, inalotayarishwa na mpishi mkuu mwenyewe. Oda yao wao imetayarishwa kwa haraka na wanafunzi walioko mafunzoni kwa sababu wapishi wakuu wako busy na oda yako mkuu. Ndio maana walihudumiwa kwanza. Tafadhali kunywa juisi wakati unasubiri."

Nilitulia na kusubiri kwa subira. Muda mfupi baadaye, chakula changu kililetwa na wahudumu 6. Kumbe Sikujua, mmiliki wa hoteli hiyo (ambaye ni rafiki yangu wa zamani aliyepotea kwa muda mrefu) aliniona nilipoingia na kuamua kunishangaza. Alibadilisha mlo wangu wa bei poa kuwa wa nyota tano. Wale vijana waliokuwa kwenye meza nyingine walishtuka mpaka wakawa wanatazamana kwa mshangao.

Ikawa sasa wao ndio wananung'unika, wakiuliza kwa nini hawakupata huduma na chakula cha aina hiyo.!!

Hayo ndiyo maisha! Watu wengine wako mbele yako na wanakula sasa, wanakucheka na kuzungumza juu ya jinsi walivyo na akili, busara na bora kuliko wewe, jinsi walivyo na connection nzuri, wamebarikiwa, wana pesa na wanafurahiya maisha.

Unasubiri bila kuchoka kwanini inachukua muda mrefu kufanikiwa, Unavumilia dhihaka na fedheha. Labda umefikiria kujiua, umepitia mfadhaiko mkubwa au una wasiwasi mwingi wa akili...!

Usijali! Mmiliki wa ulimwengu amekuona na hataki upewe mlo rahisi kama wale wanaokudhihaki. Unasubiri kwa muda mrefu kwa sababu chako ni chakula maalum. Kinachukua muda kujiandaa. Na wapishi wakuu tu ndio wanakiandaa. Subiri mlo wako kwa kutulia. Ukifika mezani hiyo sherehe ya kuchekwa na kudhihakiwa itanyamazishwa kwa Uzuri, ukubwa na utamu wa mlo wako

Mambo mazuri hayataki haraka... 2024 ni mwaka wako wa kufurahia..NAKUOMBEA

View attachment 2861548
Nimeichukua
 
Kaujumbe kazuri.......... ila kasahani umekadownlod
Aliyekula hiki chakula yupo nigeria
 
Attachments

  • Screenshot_20240104-122244_Google.png
    Screenshot_20240104-122244_Google.png
    455.5 KB · Views: 13
Amen!
Sijui kwa nini unakataa kuwa Mchungaji 😂 😂😂😂!!
Ubarikiwe! nimeipenda hii Mkuu! 🙏🙏🙏
Ila Mshana Jr ni mtata!

Ningekuwa naishi jirani naye ningepeleleza kwa siri:
1. Anakoabudu
2. Anavyofahamika anakoabudia
3. Misimamo yake akiwa nyumbani kwake
4. Jinsi familia yake inavyomchukulia
5. Anavyofahamika kwa majirani zake, n.k.
 
Juzi niliingia hotelini nikiwa na njaa kweli na baada ya kupitia menyu, niliagiza chakula.
Baada ya kama dakika 20 kundi la vijana wa kike na wa kiume waliingia na kuagiza chakula pia. Kwa mshangao wangu, watu hawa walihudumiwa kwanza kabla yangu. Niliwatazama walivyoanza kula na kucheka kimoyomoyo. Na nilimsikia mmoja wao akijigamba jinsi alivyo na uhusiano na kila mtu katika hoteli hiyo na nilihisi kudhihakiwa sana.

Niliamua kuondoka. Sikuweza kuvumilia tena, lakini mhudumu alinifuata na kuniambia kwa utulivu: "chakula chako ni oda maalum, inalotayarishwa na mpishi mkuu mwenyewe. Oda yao wao imetayarishwa kwa haraka na wanafunzi walioko mafunzoni kwa sababu wapishi wakuu wako busy na oda yako mkuu. Ndio maana walihudumiwa kwanza. Tafadhali kunywa juisi wakati unasubiri."

Nilitulia na kusubiri kwa subira. Muda mfupi baadaye, chakula changu kililetwa na wahudumu 6. Kumbe Sikujua, mmiliki wa hoteli hiyo (ambaye ni rafiki yangu wa zamani aliyepotea kwa muda mrefu) aliniona nilipoingia na kuamua kunishangaza. Alibadilisha mlo wangu wa bei poa kuwa wa nyota tano. Wale vijana waliokuwa kwenye meza nyingine walishtuka mpaka wakawa wanatazamana kwa mshangao.

Ikawa sasa wao ndio wananung'unika, wakiuliza kwa nini hawakupata huduma na chakula cha aina hiyo.!!

Hayo ndiyo maisha! Watu wengine wako mbele yako na wanakula sasa, wanakucheka na kuzungumza juu ya jinsi walivyo na akili, busara na bora kuliko wewe, jinsi walivyo na connection nzuri, wamebarikiwa, wana pesa na wanafurahiya maisha.

Unasubiri bila kuchoka kwanini inachukua muda mrefu kufanikiwa, Unavumilia dhihaka na fedheha. Labda umefikiria kujiua, umepitia mfadhaiko mkubwa au una wasiwasi mwingi wa akili...!

Usijali! Mmiliki wa ulimwengu amekuona na hataki upewe mlo rahisi kama wale wanaokudhihaki. Unasubiri kwa muda mrefu kwa sababu chako ni chakula maalum. Kinachukua muda kujiandaa. Na wapishi wakuu tu ndio wanakiandaa. Subiri mlo wako kwa kutulia. Ukifika mezani hiyo sherehe ya kuchekwa na kudhihakiwa itanyamazishwa kwa Uzuri, ukubwa na utamu wa mlo wako

Mambo mazuri hayataki haraka... 2024 ni mwaka wako wa kufurahia..NAKUOMBEA

View attachment 2861548
wananung'unika, wakiuliza kwa nini hawakupata huduma na chakula cha aina hiyo.!!
Hii ni chai ya mchunga toka Tanga, utanung'unikaje wakati haukuagiza chakula cha aina hiyo! Hata kijijini lazima useme unataka ugali au wali, hata hivyo hongera kwa kula chakula kwenye hoteli yenye mpishi mkuu na wahudumu zaidi ya sita, hongera sana sana sana.
 
Ila Mshana Jr ni mtata!

Ningekuwa naishi jirani naye ningepeleleza kwa siri:
1. Anakoabudu
2. Anavyofahamika anakoabudia
3. Misimamo yake akiwa nyumbani kwake
4. Jinsi familia yake inavyomchukulia
5. Anavyofahamika kwa majirani zake, n.k.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtani wacha utani. Chakula ulichoandaliwa kwa mpare akila lazima aaugue au hata kufa.
Mpare kazoea picha ya samaki na ugali wa mbinde umpe chakula chote hicho?Wacha utani ila kama ni motivation speech umeeleweka.
Wee mchaga tuliza mshono..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1544][emoji1544][emoji1550][emoji1550]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom