🌺 Happy Women’s Day kwa wanawake wote wa Jamiiforums!

🌺 Happy Women’s Day kwa wanawake wote wa Jamiiforums!

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
19,147
Reaction score
43,079
Kwa wanawake wote wa Jamiiforums 🌸🌸

Leo tunasimama kuwapongeza na kuwashukuru kwa nguvu, hekima, na mchango wenu mkubwa katika jamii. Ninyi ni chanzo cha upendo, ujasiri, na mabadiliko chanya kila siku.

Mwanamke si wa kusherehekewa leo tu, bali anastahili kuthaminiwa siku zote 365 za mwaka. Kila mmoja wenu ana thamani kubwa, ndoto kubwa, na uwezo mkubwa wa kuifanya dunia kuwa mahali bora zaidi.

Endeleeni kuwa na sauti, kusimama imara, kusaidiana, na kuhamasishana. Dunia inahitaji nguvu na akili zenu.

Heshima na pongezi nyingi kwenu leo na siku zote.

#InternationalWomensDay #WanawakeNguvu #Jamiifor
 
Huwa sioni umuhimu wa siku hii inayo itwa siku ya wanawake .
Hata hivyo acha nitumie upekee wa siku hii kukutakia wewe shibela matashi mazuri ya siku hii.
Nakutakia kwa moyo wa dhati kabisa.
Asante sana baraka za Mungu aliye asili ya wema wote zisikupungukie mapema
Wazungu wametuletea haya mambo tuishi nayo tu!
 
mtasifiwa na kuombewa baraka na waume zenu. Kama hamna waume mjiombee nyie wenyewe.
Omukaya, Ee siredi yako ya banhu ya Ng'waza, Tabora (Basukuma) yachile nange we bolagile 🤣🤣🤣
 
Wanawake wa nguvu humu Jamiiforums kwa upande wangu.

leo dada, Dada/Mwanamke usiye na michecheto na heka heka nyiingi nakupa 💐💐💐 yako

Binti wa zamani Dada Wane nakupa compliments zangu nyiingi, ni mtu mcheshi , unayechangamsha sana humu jukwaani, kitu ambacho wengi hawakijui wewe ni mtu mwenye akili nyingi sana 😀😀😀 mwema na huruma nyingi mnooo ❤️❤️❤️

Aaliyyah Dada /Mwanamke mwenye huruma na upole mwingi, japo siku hizi Harakati za jikoni zimepungua ni Mwanamke bora sana. Maisha yako yawe na heri nyingi na Mwenyezi Mungu akunyooshee mambo yako kama vile ulivyo wewe mwenyewe na unyoofu wa moyo wako.

Cute Wife ni Mwanamke bora sana kwa upande wangu hasa katika kutuletea habari na matukio motomoto yasiyopendelea na yanayofichua uozo, nashindwa nikuelezee vipi lakini kwa sababu ni Mwanamke wa humu Jamiiforums nakupa sifa zangu ✍️👏💎

financial services shikamoo CPA wetu, 😅😅😅 nashindwa hata nikuelezee vipi maana kuna kazi nilikua humu hukunipa ripoti. Yote kwa yote You are among the world's real Women 😍

Seran Asante kwa uwepo wako japo naona kama ni I'd mpya, huwa nafurahi kila nikiangalia notifications zangu pale juu lazima utakuwa umehusika kwa namna yoyote kwenye content yangu niliyoandika 🥳🥳🎉🎉

cocastic , Mlongo vane haijaisha mpaka iishe 😂😂😂

Lamomy Oyaaaa heri nyingii sana,🧨🧨🧨🧨

Na wanawake woote wa Jamiiforums mna mchango mkubwa na wenye thamani kubwa sana, msijisikie vibaya kutowaandika au kuwa mention.
 
Back
Top Bottom