Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
I wasn't even aware of it congrats all mamas includingi JF members.
Asante Jayfour_King; Ndo maana tupo kukumbushana. Ni vizuri sasa umekumbuka, siku bado haijaisha, si vibaya ukawakumbuka wamama ambao upo nao karibu. Nina uhakika watafurahia
Ahsante sana Mkuu.
Mimi nilipotea kidogo nikadhania kuwa ni jana. Hata hivyo ni siku muhimu sana kwa mama na dada zetu ambao wamekubali kubeba machungu mengi saaaana ili sisi tupate kuliona jua. Hakuna zawadi ya maana ambayo mtu anaweza kumpatia mamaye isipokuwa kumrudishia chembe walau kidogo ya upendo. Naomba tutafakari ni mambo mangapi tunafanya ambayo yanawaudhi mama zetu na kutesa mioyo yao? Tuwaombee kwa Mungu azidi kuwapa karama muhimu za upendo na uvumilivu.
Mamangu alinambia kuwa, ukisema kwa mfano kwamba njaa inakuuma; ni mama yako tu anayeweza kukuelewa na kuihisi hiyo njaa kama unavyoihisi wewe mwenyewe. Pamoja na kuwapenda wapenzi wetu/wake zetu, usemi huo wa mama umebaki kuwa ukweli ninao ushuhudia katika maisha yangu ya kila siku!
Ahsante sana Mkuu.
Mimi nilipotea kidogo nikadhania kuwa ni jana. Hata hivyo ni siku muhimu sana kwa mama na dada zetu ambao wamekubali kubeba machungu mengi saaaana ili sisi tupate kuliona jua. Hakuna zawadi ya maana ambayo mtu anaweza kumpatia mamaye isipokuwa kumrudishia chembe walau kidogo ya upendo. Naomba tutafakari ni mambo mangapi tunafanya ambayo yanawaudhi mama zetu na kutesa mioyo yao? Tuwaombee kwa Mungu azidi kuwapa karama muhimu za upendo na uvumilivu..
Mamangu alinambia kuwa, ukisema kwa mfano kwamba njaa inakuuma; ni mama yako tu anayeweza kukuelewa na kuihisi hiyo njaa kama unavyoihisi wewe mwenyewe. Pamoja na kuwapenda wapenzi wetu/wake zetu, usemi huo wa mama umebaki kuwa ukweli ninao ushuhudia katika maisha yangu ya kila siku!
Hongereni sana akina mama wote hapa JF na Dunia nzima!
Lakini hasa, mbali ya siku kuwa yenu, mna ujumbe gani wa jumla kwa wanawake, ambao mngependa usambae dunia nzima??
Ni matatizo gani kwa hapa Tanzania ambayo unaona ni ya akina mama zaidi katika familia, na yatasolviwa vpi?
Tuendelee kuulizana maswali haya tukisherekea!
Na ukombozi wa kweli wa nchi yetu utatokana na upendo unaotoka nyumbani (kwa mama zetu) kwani ni upendo wa asili na ni katika mazingira ambayo kuna demokrasia ya kweli. Mama hawezi kuogopa kumwambia mwanae mpenzi ukweli na hivyohivyo mtoto hawezi kusahau au kuogopa kumwambia mama njaa inauma.
mkuu DC umeongea maneno muruwa kabisa,mama ni kama wewe mwenyewe ulivyo,ndio maana hata ukiwa kibaka au jambazi siku ukiuliwa au kuchomwa moto ni mama yako pekee atakayekulilia na kusikia uchungu,kwangu mimi mama ni kila kitu kwakweli,nilishangaa na kusikitika pale niliposikia mwanamuziki niliyekuwa namshabikia sana FALLY IPUPA
alimuua mama yake kwa uchawi ili apate umaarufu,inawezekanaje?ila haya mambo yapo