Invisible,
Nashukuru sana kwa kutuweka live hapa kijiweni katika kipindi cha mwaka mzima wa 2008pamoja na suruba zake, toka Jamboforums had Jamiiforums. Nakutakia sehere njema za Noel na maadhimisho ya mwaka mpya wa 2009.
Katika kipindi hiki tunachoelekea kumaliza mwaka wa 2008 na kuanza mwaka wa 2009, ni vyema tupitie tena mijadala mikubwa iliyofanyika hapa tuone ni ipi ilikuwa na mafaniko na ni ipi haikuwa na mafanikio. Vile vile tujifunze ni kwa nini hatukufanikiwa na ni kwa nini tulifanikiwa kusudi tuweze kuongeza ufanisi zaidi katika mijadala ya mwaka mpya wa 2009.