Ila wanawake nyie Mungu atuongoze vizuri tu tuishi nanyi kwa akili.
Sikukuu yenu ikifika...hata malaya na waliowabambikia baba zetu mimba tunawatakia.
Ila yetu mnaanza ubaguzi mara wanaochepuka mara sijui waliofanya nini.
Baba yeeyoooo, takwinyaaa
Aaahahahahhaaa asante kunipa cheko la jioni, habariikoo!!
Sasa baba yeyoo vile wajua wanaume nyie huwa mko straight hamna mambo mob wala mambo za kona kona. Si waonanga hata mkienda kwa shop, ukiuliza hii shati iko ngapi, ukiambiwa chapaa 20 unatoa na wala huulizi punguzo la bei au ati ilitengenezwa wapi au inakaribia ku expire lini ama kuna rangi gani na gani.
Ila sie sasa, hili shati bei gani... looh bei kubwaa punguza basii, bei itapungua kiasi halafu unajisemesha mmmhh kwani kuna rangi nyingine, utatolewa rangi zote, kisha utajisemesha tena sijui atalipenda... kisha unauliza tena, naweza kuja kubadili kama lisipomtosha au asipopenda hii rangi, najibiwa kisha najiwazisha tena halafu nasahau kama nilishaomba kupunguziwa bei naanza upya, sasa baba angu leo sijabeba hela ila kesho au keshokutwa narudi kuja kulichukua, au nikija nije nae ajaribu kabisa. Wauzaji wananitazama na kuanza kurudisha nguo, nikiwa naelekea kutoka dukani narudi tena kuuliza, hivi mna suruali ambazo zinafaa na kuendana kuvaa na hilo shati......!!!🤣🤣🤣 kama si kufukuzwa muuzaji anashika simu kama vile anaongea na simu hadi niondoke au aingie mteja mwingine.
Ila mie nawapenda wanaume, hasa wale magentomani.
Sasa, choma wapi leo..?