Happy Birthday To you

Happy Birthday To you

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,295
Reaction score
60,915
Heeey,. Hope you good.
Najua haiwahusu lakini leo ni birthday ya wazazi wangu wote wawili😍😍😍.. ( Wanashare birthdate lakini kila mmoja na mwaka wake)... But naandika huu uzi special kwajili ya Baba yangu Cause najua atasoma kwasabu yupo humu,.


Dear Dad,. As we celebrate your 65's birthday natamani ujue kuwa mimi Leejay mwanao nakupenda na nina kuombea uendelee kuishi miaka mingine mia na zaidi ya hiyo .. Kwasababu uwepo wako kwangu na ndugu zangu unamaanisha kila kitu kwenye hii dunia iliyojaa watu wengi wenye chuki na roho za Ajabu..

Nakushukuru kwakua siku zote umekuwa bega langu,. kiongozi wangu , mwalimu wangu, mtetezi na shujaa wangu katika kila vita ninayopigana ... kwako ndio sehemu pekee ninajihisi nakuwa na amani hata nipitie magumu kiasi gani,. Ni wewe pekee ambae umekuwa unaniamini na kunisupport hata kwenye yale ambayo kwa nguvu zangu nasema siwezi,.

Ni wewe pekee umenifanya nijitambue mimi ni nani na ninatakiwa kuwa nani,. Na kila siku unanithibitishia hilo kwa vitendo,. Niko hivi nilivyo leo kwasababu yako baba yangu.. Wanasema kwenye mafanikio ya kila mwanamke basi kuna mwanaume nyuma yake,. Yes ni wewe mzee wangu ambaye always umekuwa ngazi yangu ya mimi kupanda kila hatua nayoipiga kwenye maisha yangu..

Najua umejinyima vingi sana kwajili yangu na ndugu zangu,. But deep down ni mimi ambaye nimekufanya uishi hata maisha ambayo hukufikiria kuishi kwasababu mimi mtoto ambaye nimekusababishia matatizo na mambo mengi sana angekuwa mzazi mwingine tayari angeisha nipa laana😭😭😭 lakini wewe Baba yangu hujawahi kunikatia tamaa wala kunitamkia neno lolote baya zaidi umekuwa ukinikanya na kusimama upande wangu pale ambapo kila mmoja alionyesha kutokunihitaji tena...

Najua kama mtoto kwa mzazi nimekukosea mambo mengi sana kwa kujua hata mengine kwa kutokujua lakini kwako hayajawa na maana yoyote zaidi umeyafunika kwa upendo wako.. Nisamehe sana Baba yangu🙏🙏

Kwa ulipofikia nilitamani nikufanyie mambo mengi sana makubwa lakini siwezi kwasababu mwanao bado sijawa vile umetaka niwe,. Lakini napambana na nahaahidi haitachukua mda mrefu kila kitu kitakuwa mahali pake shujaa wangu,. Kwa umri wako saizi ulitakiwa walau uwe na watu wanakuita babu but haijakuwa hivyo.. Though hili ni kosa lako, ungetuzaa mapema saizi ungekuwa nao wakutosha😂😂😂😂.. Ni kwamba kama vile ambavyo sisi hatujateseka tunaandaa mazingira pia na wajukuu zako wasije kuteseka...

Ninayo mengi sana ya kuandika lakini wacha niishie tu hapa nisije kujaza saver za Jf,. Nakuombea uishi miaka mingine mingi zaidi uushangaze ulimwengu,. wewe ni zaidi ya shujaa kwenye maisha yangu..

HAPPY BIRTHDAY...
 
Back
Top Bottom