Happy birthday inanisulubu

Happy birthday inanisulubu

madala mujipa

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
1,421
Reaction score
864
Amani kwenu wadau

Juzi kati ilikua ni kumbu kumbu ya siku ya kuzaliwa mamsapu,sasa kulingana hali ya maisha ni ngumu ,na yeye kulipokucha aliniambia baba timdwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa nataka unifanyie kijisherehe nifurahi na shoga zangu ,imekua mimi nakwenda kwa wenzangu kila mara lakini kwangu hakuna,

Ok mimi sikubisha kiume nikaenda kwenye mizunguuko yangu nikanunua keki na vitu vingine vitafunwa nikanunua kreti kama mbili za soda nikarudi navyo nyumbani,nikakuta familia yote wameunganika nikatuma mwanangu ashushe vile vitu avilete ndani,mamsapu akauliza vitu hivi ni vya hiyo sherehe.. nikamjibu ndio,ukumbi wapi ..aah nikamwambia ukumbi, mbona nyumba yetu inatosha tu,..akauliza na hao shosti zangu..mimi nikajibu shosti zako si hawa wanao wanatosha mpaka ubebe watu wakati mambo sio freshi,

Baada ya hapo bibie akaingia ndani kanuna kalala hataki mazungumzo,na hata tendo la ndoa pia nisimguse yaani tafrani na inashangaza utamaduni huo alikua hana miaka nenda,hili la kunyimwa haki kisa tu birhtday pananitatiza

Sasa jamani naona giza nisaidieni mawazo kidogo tu!
 
Huyo mke wako ana umri gani mkuu? Maana kama ana kautoto flani hivi..
 
Naomba picha ya keki na kreti la soda tafadhali
 
Kwa tabia hizo basi ruksa kumpatia msaidizi ningekuwa dume nikaoa ke mpenda shughuli za kipuuzi Halafu eti anazira angejuta walahi
 
Duh sasa shida hapo nini?

Toka nenda kusipojulikana. Rudi late. Lala kimya. Kesho yake amka mapema nenda kwenye mishe.

Ukiuendekeza huu upuuzi itakula kwako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom