Ndugu wana-MMU leo ni krismasi tunapokumbuka kuzaliwa kwa Mwokozi wa ulimwengu Yesu Kristo. Nawatakia kila la heri katika siku hii. Lakini vilevile ni siku ya kuzaliwa kwa mwana-jukwaa mwenzetu dada christine Ibrahim. Binafsi nimshukuru Mungu kwa afya njema na uzima ambao amemjalia huyu binti. Yeye mwenyewe anayajua maisha yake alikotoka na alipo leo. Ninachomuomba ni yeye kukaa na kutafakari ukuu wa Mungu maishani mwake. Kama bado hajaolewa namtakia kila la heri, kama bado hana kazi basi Mungu atende juu yake, pamoja na mipango mingine mingi maishani mwake. Unachotakiwa kufahamu christine Ibrahim ni kuwa Mungu atabaki kuwa Mungu na usikome kumuita maishani mwako. Zaidi christine Ibrahim washukuru wazazi wako kwa kukulea mpaka leo na ukumbuke na wewe kuwatunza ili utimize ile amri ya Mungu ya kuwatii wazazi wetu. Na mwisho christine Ibrahim kumbuka kuwapenda wote wanaokuzunguka kuanzia nyumbani mpaka JF. Kila la heri na sikukuu njema. Amen:israel: