HAPPY BIRTH DAY Frédéric Chopin; | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HAPPY BIRTH DAY Frédéric Chopin;

Discussion in 'Sports' started by Steven Sambali, Mar 1, 2010.

 1. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #1
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Hii video hapa chini ni mashindano ya Chopin hapa Warshava mwaka 1995 ambapo kijana wa Kirusi aitwaye Alexei Sultnov (RIP) alipiga kijanda hadi nikampenda ingawa sikuwa mpenzi wa Chopin. Ila kwa jambo ambalo hadi leo sielewi, walikataa kutoa nafasi ya kwanza na wakasema wawili wameshika nafasi ya pili. Sultanov aliikataa nafasi ya pili kwani aliamini (wengi tuliamini) kuwa alikuwa kapata nafasi ya kwanza.

  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=Yps4hKjt8cE"]YouTube- Alexei Sultanov -Warsawa Recital part.4,Chopin Fantasie Impr[/ame]
   
 2. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #2
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Leo hii hapa Warsaw (Warszawa au Warshava) wamefungua jumba la makumbusho la huyu Chopin katika kusherehekea miaka 200 tangu kuzaliwa kwake. Jumba hilo limefanywa la kisasa saaana kiasi kwamba kweli lipo karne ya 21. Mfano kuna sehemu ukiweka kitabu che NUTA za mziki wa Chopin, basi kinanda kinajipiga chenyewe.

  Kwenye lile jumba la Thieta ambalo kama sikosei ndiyo la taifa na kubwa kuliko yote, kuna concert kubwa sana na wamekuja wapiga vinanda wengi maarufu duniani. Nafikiri bei yake haitakuwa nzuri sana kwa walalahoi.

  http://blog.taragana.com/e/2010/03/01/new-chopin-museum-opens-in-warsaw-composers-home-city-on-his-200th-birthday-95461/
   
 3. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  aminia kaka unajua kumchambua huyu jamaa...duh heko yake na mungu amlaze mahali pema peponi...Wapolo wabaguzi ndo maana hawakumpa Mrusi ....
   
 4. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #4
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45

  Mkuu, nisingelipenda sana kutumia neno WABAGUZI. Ni kweli wana mapungufu yao ingawa tangu waingie EU kwa sasa wanabadilika sana. Timu zao zimejaa weusi kibao na moja ya timu maarufu hapa Poland/Warsaw iitwayo LEGIA, moja ya ma-Captain wa timu hiyo ni jamaa aitwaye Dickson Chotto ambaye pia ni beki wa timu ta Taifa ya Zimbabwe. Pia kama ulimuona Kalu Uche huko Angola, jamaa kachezea sana hapa Poland, mji wa Krakow na baadaye akahamia hapa Warsaw.

  Nirudie tena kuwa ni kweli wanamapungufu yao ila kwa sasa wanabadilika sana. Kwa mfano zamani ukipata kesi na Mpolish basi una hali mbaya. Ila tangu waanze kushtakiwa kwenye mahakama ya Ulaya na kushindwa kesi karibu zote na hapo kulipa fidia kubwa sana, wameanza kuwa wakali na waangalizi wa sheria. Nimeshashuhudia club, Mweusi karuhusiwa kuingia na Mpolish kakataliwa na sababu eti jamaa ni MREFU.
   
 5. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  sasa kwa nini hakupewa kuwa mshindi na jamaa ni mkali sana hata ukiangalia Wikipedia anatoboa kweli lkn poa poa..RIP alex..
   
 6. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #6
  Mar 2, 2010
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Magulumangu,
  Ni kweli kijana Alex alikuwa mkali sana na alizibeba roho za Wapolish wengi. Tatizo ni kuwa ile kamati ya maandalizi na usimamizi wa hayo mashindano pamoja na hivyo vizee Vi-Profesa vya mziki, ndiyo vilikuwa vikoministi na roho korosho sana. Vilikasema eti hakuna mtu aliyefikia upigaji wa juu hadi apewe nafasi ya kwanza. Ilikuwa kichekesho kwa sababu walikuwa wanashindanishwa watu na si watu wanashindana kufikia usawa fulani.

  Huyu kijana Alex alikuwa ni Chain Smoker mkubwa sana. Alikuja kuuguwa sifahamu hadi leo ni nini kwa sababu sikufuatilia sana ila kuna wale Wapenzi wake hapa Poland walikusanya hela ili zipelekwe Russia zimsaidie katika matibabu. Labda ndiyo uzuri na ubaya wa mambo mengine kwani kama si kudhurumiwa ushindi, labda tungelikuwa tumeshamsahau.

  Wafaransa nao wamesherehekea Bday ya Chopin:
  http://www.english.rfi.fr/culture/20100301-paris-celebrates-chopins-birthday
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...