Hapo zamani

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
HAPO ZAMANI HALI HAIKUWA KAMA HIVI:

HAYA YOTE TUNAYOYAONA HAYAKUJA KWA MIUJIZA. HATUNA BUDI TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUWA WAPO AMBAO WALIJITOA NAFSI ZAO KUTUMIKA NA KUIFANYA HALI IWE KAMA HIVI TUNAVYOWEZA KUONA HII LEO. WENGI WAO HATUNAO TENA.
Cathedral.JPG

http://dsmarchdiocese.catholicweb.com/index.cfm

MWENYEZI MUNGU AWAREHEMU KWA KADIRI YA MAPENDO YAO!.

Hapo zamani: hili ndilo kanisa na lori lillilotumika na Wamisionari.

Wakati huo magari yalikuwa ni ya gharama sana na maeneo mengi yalikuwa hayapitiki kwa magari kwa sababu ya vijinjia vidogo. Hivyo waliweza kutumia pikipiki kwa kusafiri mbali zaidi kutoka kituo kimoja hadi kingine.

Mmoja mwa watawa Waafrika wa kwanza

Picha inaonyesha mwanzo wa kuuguza wagonjwa hapa Peramiho, masista wa Ulaya na masista wa Afrika wabenediktini walikuwa wanatibu vidonda.

Abasia Peramiho
 
Hii hali mbona bado ipo?? Sikuelewi unaposema hapo zamani! Kama ni vinjia vyembamba ni uzamani basi kwetu tuko zaidi ya zamani, hayo makanisa ya nyasi na nyumba za kulala za nyasi bado ni sehemu ya maisha ya baadhi ya watanzania. Hata hapo kale ilikuwa ni baadhi ya Watanzania
 
Wow, umenikumbusha mbali, unajua huu ndo mkoa niliopatia elimu yangu, huko mpitimbi na mbiga yote iko mkononi mwangu...peramiho mission ni mwenyeji pia, songea town ndo usiseme, tulikuwa tunaenda kuzurura shule ikifunga au weekend (tena kwa kutoroka wakati mwingine)...kweli tumetoka mbali.
 
Ni zamaini za historia ya Kanisa mzee.

Kanisa kuu la mtakatifu Joseph lilijengwa chini ya usimamizi wa Padre Maurus Hartmann ili wasaidia Maaskofu wa Kibenediktini Askofu Cassian Spiss na Thomas Spreiter kama kanisa kuu, hadi waingereza walipomfukuza Askofu Thomas mwaka 1920.

PERAMIHO CATHEDRAL CHURCH:

Humu ni upande wa ndani wa kanisa mnamo mwaka kama 1911. Hilo lilijengwa kama kanisa la muda tu (Kijerumani liliitwa "Notkirche", maana yake "Kanisa la dharura").

Kanisa dogo lilitumika kuanzia mwaka 1913 hadi mwaka 1948.

Maandalizi ya ujenzi

Ndivyo ilivyo sasa.
 
Wow, umenikumbusha mbali, unajua huu ndo mkoa niliopatia elimu yangu, huko mpitimbi na mbiga yote iko mkononi mwangu...peramiho mission ni mwenyeji pia, songea town ndo usiseme, tulikuwa tunaenda kuzurura shule ikifunga au weekend (tena kwa kutoroka wakati mwingine)...kweli tumetoka mbali.

Wapi, Box 2, Hanga, Major Seminary, Ruvuma, Kigonsera (Kaigo), Likonde, Hagati, Lundo, Liuli St. Paul) Kindimba, au Maposeni?
 
Wapi, Box 2, Hanga, Major Seminary, Ruvuma, Kigonsera (Kaigo), Likonde, Hagati, Lundo, Liuli St. Paul) Kindimba, au Maposeni?

Kaigo mkuu, tulikuwa karibu na seminari ya Likonde, si unajua ile shule ya kigonsera ndo tulikuwa tunapata ujiko ati ndo amesoma mkapa....kitimoto yetu tulikuwa tunatafunia pale harare centre..wow...na ndizi choma fulani ivi...siku ingine tukafuata mbuzi wa sherehe Lupilo...raha tupu...na vidude fulani hivi virefu vya mviringo wanatengeneza mfano wa maandazi wenyewe wanaita jina baya ati "vimbolo"..ukikatiakatia kwenye uji na blue band, wanafunzi wenzio lazima wakufuatefuate..hahaha, shule ilikuwa imezungukwa na maembe yale ya songea, ikigonga kengele ya saa nane kwenye lunch, kila mtu utamkuta kwenye mwembe juu anaangua apendavyo...asubuhi dagaa/njuka (form one) kazi yao ni kusafisha maembe yaliyodondoka njiani kwani ni uchafu...yaaniii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom