Watu wa zamani #8

Watu wa zamani #8

kafumo

Member
Joined
Aug 30, 2026
Posts
26
Reaction score
15
Kwenye uwili sehemu moja iko na miundombinu au taratibu za siri sana zinazo fanya kuwepo kwa sehemu nyingine.

Watu wa zamani waka chukua mifano miwili mmoja wakaangalia jinsi mti ikiwa utalazimishwa mizizi ionekane bayana na macho unavyo poteza uhai wake, wa pili wakaangalia jinsi mimba inavyo tengenezwa ndani na jinsi ikiwa mtu atakata tumbo ili kuona inavyo weza kuwa hatari kwa mama na mtoto aliye ndani hata kupoteza uhai.

Basi wakaheshimu sana uhusiano mkubwa uliopo baina ya sehemu mbili za sheria ya uwili.

Wakaelewa kuwa katika uwili kila sehemu ina mambo yake na mambo ya sehemu yoyote yanaweza yasitambuane moja kwa moja isipo kuwa kwa utaratibu maalumu sana.

Sehemu moja ya uwili wakaona ni bayana kabisa na sehemu nyingine ya uwili wakaona ni sirini, watu wa zamani wakaendelea kusema sirini ndio sehemu yenye mambo mengi sana yanayo fanya uwepo na umilele wa bayana, na hivyo sirini ndio chanzo mama cha elimu na maarifa yaliyo hifadhiwa kwenye hazina za watu wa kale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom