Hapa Zitto ana maanisha nini?

Hapa Zitto ana maanisha nini?

..mimi siyo mtaalamu wa ujenzi wa reli.

..sasa kwasababu wewe ni mtaalamu nilitegemea ungenielimisha / ungenisomesha kuwa Tazara walikuwa wakifanya "a" lakini sgr tunafanya "b".

..Nilitegemea uzifanyie mlinganisho reli hizo mbili na kutueleza kwanini moja ichukue muda mrefu zaidi kujenga kuliko nyingine ukizingatia kwamba teknolojia imekuwa bora zaidi miaka hii.

..Tazara pia inayo madaraja na mahandaki makubwa. Kwa hiyo jicho langu ambalo siyo la kitaalamu bado nina maswali mengi.

..I am just trying to get more clarification from you. Sina uhakika kama kuna mwanachama mwingine wa JF anayeweza kutupa maelezo ya uhakika kama yako.
Kwa kweli sina data zozote za mradi wa TAZARA ili niweze kulinganisha na mradi wa SGR. Kama kuna engineer wa TAZARA humu jf, atuwekee hapa.
 
Kwa kweli sina data zozote za mradi wa TAZARA ili niweze kulinganisha na mradi wa SGR. Kama kuna engineer wa TAZARA humu jf, atuwekee hapa.

..Asante kwa majibu yako.

..maswali haya nadhani unaweza kuyajibu.

1. Kipande cha Dar - Moro kitakwisha lini?

2.Kipande cha Moro - Makutopora kitakwisha lini?
 
..Asante kwa majibu yako.

..maswali haya nadhani unaweza kuyajibu.

1. Kipande cha Dar - Moro kitakwisha lini?

2.Kipande cha Moro - Makutopora kitakwisha lini?
Pamoja na changamoto za mvua zinazonyesha tangu mwezi Oktoba 2019 na kuathiri kwa kiwango kikubwa work progress, nina uhakika kipande cha Dar - Moro kitakwisha mwaka huu 2020.

Moro - Makutopora, sifanyi kazi kipande hiki hivyo sina uhakika ni lini kitakwisha.
 
Huyo jamaa keshajitoa ufahamu. Hata umwambieje yeye atapinga tu. Watu kama hawa ni wa kuwaacha kama walivyo.
 
..Asante.

..Unadhani kipande cha Dar-Moro kitajiendesha kibiashara, kwa faida, na kutoa uwezekano wa kurudisha fedha zilizowekezwa?
 
Huyo jamaa keshajitoa ufahamu. Hata umwambieje yeye atapinga tu. Watu kama hawa ni wa kuwaacha kama walivyo.

..sasa maswali niliyouliza yana ubaya gani?

..kutaka kujua reli ya Dar-Moro itakwisha lini ndiyo kupinga?

..Au kutaka kujua kama reli itaendeshwa kibiashara na kwa faida ni sawa na kupinga mradi wa reli?

..inawezekana uko ktk kundi la kusifia bila kujua faida za unachokisifia na kukiunga mkono.
 
Hiyo reli sio ya kukamilika Leo wala kesho nyie mapimbi,acheni kudanganya watu na video uchwara zenu.
 
Je, unaweza kutuwekea nakala ya BOQ ya mradi wa TAZARA ili tulinganishe na SGR ili tuone scope of works zinatofautina kwa kiasi gani. Kwa mtazamo wako scope of work unaitazama in terms of kilometres pekee yake. Earthwork quantities (fill and cut volumes) na quantities za concrete na nondo (reinforcements) kama ni kubwa (nyingi) zinaweza kuchangia sababu ya mradi kuchukua muda mrefu kukamilika.
Kwenye mradi wa sgr kuna work items tena kubwa ambazo nina uhakika haziko kwenye mradi wa TAZARA, mfano: madaraja ya juu kutoka Dsm station hadi Ilala, daraja kubwa la mto Ruvu, electrification and catenary works, nk. Yote hayo yanafanya design za miradi hii miwili itofautiane na pia scope ya kazi itofautiane!
Lakini pia ikumbukwe kwamba, huwa kuna changamoto nyingi sana wakati wa utekelezaji wa miradi mikubwa kama huu wa sgr.

Sisi tuko huku Shinyanga, hatuoni hata dalili kuwa reli hii inajengwa....

Hata kuwaona tu wale surveyors wa kuzuga kuzuga kisiasa, hatujawaona....!!

Nadhani kama na hii inayopita hapa Shinyanga itajengwa kwa kiwango cha SGR, labda miaka kumi au ishirini ijayo kwa sababu maandiko ya kutafuta mkopo kwenye mabenki bado yanaandaliwa, right?
 
..sasa maswali niliyouliza yana ubaya gani?

..kutaka kujua reli ya Dar-Moro itakwisha lini ndiyo kupinga?

..Au kutaka kujua kama reli itaendeshwa kibiashara na kwa faida ni sawa na kupinga mradi wa reli?

..inawezekana uko ktk kundi la kusifia bila kujua faida za unachokisifia na kukiunga mkono.
Lini ukarabati wa makao makuu pale ufipa yataanza?
 
Kipande cha barabara ya mayoni Tabora na kile cha tabora urambo na kila cha kaliua kigoma tumekuwa ni hadith za lumumba.zisizoisha kama hadith ya kuwawa kwa alphonso mawazo na kubambikiwa case kwa kina KABENDERA kisha wakilipa wananunua uhuru wao! Eh likichaa la magogoni

Sent using Jamii Forums mobile app
Shauri yako, siwezi kukusaidia.
 
Back
Top Bottom