Ndugu, kwenye ujenzi wa reli track works ni kazi ndogo sana. Kazi kubwa iko katika kusawazisha milima na mabonde (earthwork - fill and cut works) pamoja na ujenzi wa madaraja.
Fill work ni ujenzi wa tuta
Kwa mfano: kuna section panatakiwa lijengwe tuta la kimo (height) meta 20 au zaidi. Procedure ni kwamba tuta hilo linajengwa kwa tabaka (layer) lenye unene wa sentimeta 25 (selected material, well mix with proper moisture, well compacted followed by inspection and testing). Meta 20 ni sawa na tabaka (layers 80). Kwa urefu wa kilometa 1 hii kazi ili ikamilike inaweza kuchukua atleast 35 days (kwa kufanya kazi usiku na mchana ukiwa na 3 sets of equipment, mvua isiponyesha hata siku moja, without equipment breakdown au tatizo lolote lile).
Kwenye mradi huu wa SGR-Tz, track works tabaka hazizidi 3 ambazo kila tabaka unene wake hauzidi sentimeta 30, kisha wanaweka ballast (kokoto nene), mataruma (sleepers) na hatimaye kuweka reli (vyuma). Track works kwenye urefu wa kilometa 1, kazi zote hizi zinaweza kukamilishwa ndani ya siku 5.
Progress report inayotolewa na TRC inaandaliwa na Msimamizi wa mradi ambaye ni KOREA RAIL ROAD (KORAIL JV) na ni taarifa sahihi. Kuamini au kutokuamini taarifa hizi ni uamuzi wako na haulazimishwi kuamua vyovyote vile.
Mimi niko site kila siku kwenye mradi huu tangu 2017, ninajua kinachoendelea na taarifa zinazotolewa kuhusu maendeleo ya mradi ni sahihi.