Hapa Sijamuelewa Lukuvi

Badala ya kumuuliza Chris Lukosi ana maana gani anaposema Dj na Dr, badala yake, baadhi ya watu wanaanza kumlisha maneno na kumshambulia bila hata ya kufahamu maana ya bandiko lake.

Kama ilivyo kwa mleta mada, hata baadhi ya wachangiaji nao wanaonesha tatizo lile lile lililomtatiza mleta mada. FAUX PAS
 
Last edited by a moderator:
Hivi kumbe nimetukana mtu hapa?
Nimetaja jina la mtu?
Usipende kujikomba namna hii
Wangoni hawako hivyo
Wahehe kama wewe ukifa unazikwa na kijinga cha moto makalioni...hakuna Wahehe wanafiki kiasi hicho
 
Kama hujaelewa ni vizuri kutokuchangia mada kuliko kuchangia usichokielewa,mtoa mada ameeleza waziwazi na anauliza LUKUVI anataka jengo libomolewe kwa kuwa limejengwa na the same contractor au kuna sababu za kiufundi? Kama unajuwa mojwapo ya hilo uje na jibu sio kuchangia usichoweza.
 
ni upuuzi kufanya unachokifanya hana kitu unajua wewe, anaagiza yeye mbona waziri wa ujenzi ajazungumza? huna lolote
 
Agizo la lukuvi liko sahihi kwa maslahi mapana ya maisha ya watanzania
 


Usifikiri kila anayepinga hoja humu ni upinzani,mbona ufahamu wako unaonekana ni mdogo sana,Wa wapi wewe!! Lukuvi mara nyingi amekuwa mdandia hoja na mkurupukaji,Suala hili linahitaji uchunguzi kwanza.Shughulisha Akili! Kwani ni lazima ukubaliane na kila hoja ya kiongozi kisa anatoka chama chako.Pima Hoja tafakari siyo lazima uchangie kila Post.Acha Uzuzu.
 

Chris Lukosi acha mambo yako ya ajabu ajabu hapa, kama hujui uliza ufahamishwe sio unakurupuka tu hapa na kuanza kumshambulia mleta mada pasipo sababu.

*Mleta mada ameuliza pale ambapo hajaelewa, wewe una rush kumpa Itikadi ya Chadema na kisha hapo hapo unawatukana matusi ya nguoni viongozi wa Chadema.
Yaani pamoja na kuwa uko UK lakini bado ustaarabu na upeo wako viko chini sana.

*Issue ya viongozi wa Chadema kufika eneo la tukio mbona iko wazi kabisa, Mbowe alifika siku ile ile ya tukio na akaongea maneno ya hekima na busara kubwa sana, Kisha John Mnyika naye alifika eneo la tukio na kushirikiana vema na vikosi vya uokoaji.

*Hoja ya msingi inabaki pale pale;
1/Kama Mfalme(Kikwete) kafika mara tatu katika eneo la tukio bila kutoa kauli, kisha Bosi(Pinda) kakosa la kusema/Kuamrisha, inakuwaje Karani asiyehusika(Lukuvi) atoe amri tena mbele yake?

2/Ni uchunguzi wa kitaalamu kiasi gani umefanyika mpaka Lukuvi aje na 'Straight Decree' ya kusema Ghorofa livunjwe tena haraka sana?

3/Lukuvi ana mamlaka gani ya kiserikali/Kisheria kuweza kutoa amri ya namna ile ya kusema ghorofa livunjwe?

4/Nini kitatokea kama Rais, Waziri mkuu au Waziri wa Nyumba na makazi watakuja na agizo tofauti na Lukuvi?
 
Last edited by a moderator:
Livingstone Lusinde
TANURU LA FIKRA (DAKIKA 10 ZILIZOPITA LEO)



Mwalimu nyerere aliwahi kusema nanukuu" Mshahara wangu mnajua ni shillingi ngapi? ni tsh 5000, katika nchi maskini, je mnajuwa itamchukua muda gani kwa maskini anayepata tsh 200 kwa mwezi kuufikia mshahara wangu??, itamchukua miaka 25" mwisho wa kunukuu .swali la kujiuliza leo hii million 47.8 anazopokea rais wetu , itachukua muda gani mwalimu, nesi , polisi na watumishi wengine kuufikia??, mwalimu nyerere na sokoine waliliona hilo na wakashusha mishahara yao , mwalimu alishusha kutoka 5000 mpka 2500 na sokoine alitoa nusu ya mashahara wake akawa gawia watumishi wa chini , ili polisi aufikie mshahara wa rais wa leo anatakiwa afanye kazi miaka 33.5 na watanzania wako kimya tu wao kazi kulalamikia mishahara ya wabunge tu na sijawahi sikia hata mmoja analalamikia mshahara wa rais na marais wastaafu ambao bado wanalipwa 85% ya mashahara wa rais aliyeko madarakani
 
Hivi kumbe nimetukana mtu hapa?
Nimetaja jina la mtu?
Usipende kujikomba namna hii
Wangoni hawako hivyo

Lukosi sijawahi na wala sitarajii kujipendekeza kwa mtu coz hiki mungu alichonijalia kinanitosha na familia yangu.Hapo kwenye red umetaja Dr na DJ nafikiri unajua kabisa unaowamaanisha.
Lengo langu lilikuwa ni kukumbusha kama binadamu mwenzangu kuwa Mungu hapendi tuishi hivyo..........Ogopa kumtukana Mtu ambaye yeye akujibu na wala usimfanyie mtu kitu kibaya....hivi unawakumbuka kina Mashishanga and the like 2005 walichomfanyie JK, Mangula amshukuru sana Mkapa.Hiyo ni mifano michache tu ambayo majibu yake ya hapa hapa duniani.
 
Tujiandae watanzania kulipa faini kwa kodi zetu pindi mwenye jengo atakapo enda mahakamani
 

Tamko lililotolewa na Lukuvi ni ushauri uliotolewa na wataalam baada ya kukagua jengo, Tamko hutolewa na mtu mmoja (Serikali) baada ya kushauriwa na watendaji haiwezekani kila mtu alonge lake
 

Najua umemuelewa kwamba hajielewi kwa kuwa haelewi anachosema wala anachokifanya. au labda anajua kutimiza kile alichotumwa. Si ni lukuvi aliyemaliza form 4 thru QT juzi, au ni mwingine!!!?
 
Hawa ndo vichwa wa CCM.
CCm ipo juu kama Lukosi na William Malecela.

:rockon:
 
Tamko lililotolewa na Lukuvi ni ushauri uliotolewa na wataalam baada ya kukagua jengo, Tamko hutolewa na mtu mmoja (Serikali) baada ya kushauriwa na watendaji haiwezekani kila mtu alonge lake
Acha kutulisha sumu hapa
*Ni wataalamu gani wa majengo walilikagua hilo jengo(Kikwete? Sadiq? Kova? Mbatia? Lukuvi?), lini wamefanya hivyo na lini na wapi walitoa ushauri huo
(Kumbuka wataalamu wakuu wa ujenzi wa jiji walikamatwa na wengine wanatafutwa, nguvu na akili zote za watawala zilikuwa kwenye kuondoa kifusi na kuuokoa majeruhi, sasa sijui lini waliamua Kuconcetrate kwenye ukaguzi wa hayo majengo?)

*Kama Waziri mkuu(Pinda) anasema Hana chochote cha kuzungumza, Lukuvi anapata wapi jeuri ya kuzungumza hayo tena mbele ya Pinda?
 
1. Kubomolewa kwa jengo jirani kunaweza kuwa ni kwa sababu ya madhara kwenye jengo hilo yaliyosababishwa na jengo lililobomoka

2. Cha ajabu ni suala la kumtia mbaroni mchora ramani. Yeye ana kosa gani? Yeye anapewa maagizo. Engineers ndio wenye kazi ya kutafsiri ramani kuwa "structural reality", na kupata vibali vinavyotakiwa.

Lakini usishangae sana ya Lukuvi, kumbuka kwamba kwanza ni nguini anaetoa amri zinazohusu kazi ya uhandisi; pili hata degree zake za unguini ni feki. Sasa unategemea nii hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…