Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Waziri wa mambo ya ndani ametoa agizo kwamba kiongozi wa Act, Zitto, akamatwe kwa "kufanya" mkutano wa hadhara nje ya jimbo lake.
Ukifikiria, inawezekana kabisa kwamba Zitto alifanya hivyo makusudi ili hili suala la wabunge kutohutubia nje ya majimbo yao liweze kupatiwa ufumbuzi wa kisheria katika mahakama. Japo Lugola ana background ya sheria, anaweza akawa ameingia kichwa kichwa katika hili na kujikuta anaangukia pua, na kuumbuka yeye, rais na serikali ya CCM kwa ujumla. Mambo makubwa matatu yanayoweza kufanya Lugola aangukie pua ni yafuatayo;

- Kwanza Zitto hakufanya mkutano wa hadhara, bali alialikwa katika mkutano halali wa hadhara
- Zitto ni kiongozi wa kitaifa, na uongozi wake wa kitaifa unampa wigo wa kufanya kazi yake ya kisiasa sehemu yoyote hapa Tanzania
- Hakuna sheria ambayo inamkataza mwanasiasa nchini kufanya mkutano wa hadhara popote nchini, na katiba inaruhusu hilo, hasa ikizingatiwa kwamba tamko la rais halina nguvu ya kisheria, na pale tamko la rais linapopingana na sheria basi mahakama zitatoa uamuzi kulingana na sheria, sio tamko la rais.
Last edited by a moderator: