Hapa ndipo wanawake wengi tunapofeli

Hapa ndipo wanawake wengi tunapofeli

Mapenzi yatatuua jamani, wanawake wanawaliza sana wanaume wenzangu, haha
 
Unaweza kuwa ushauri mzuri kwa wanawake ambao wana akili na wako kwenye ndoa saa hii
 
Kitu ambacho wanawake wengi hawajui ni kwamba, mwanaume unaweza kumuibia pesa nyingi tu, ukamuharibia vitu vyake vya thamani e.t.c , lakini mwanamke asijaribu wala kudhubutu kutembea na mme mwingine tena mpaka mimba na akagundua, kusamahewa na ngumu sana, mwanaume akishaingiliwa kwenye himaya yake namna hiyo, msamaha ni mgumu sana kwake kutoa. Namshauri huyo mwanamke ampe huyo jamaa muda wa
yeye kuondoka hapo na kurudi kwao kwanza.
 
Mwanamke Kama mwanamke uliyeolewa na mwanaume wako akakuheshimisha tulia visasi havisaidii badala yake vinabomoa

Angalia hapa: Mwanamke unaamua kulipa kisasi kwa mumeo kwa kucheat kwa sababu na yeye alikucheat

Unaamua kumnyima mumeo unyumba kwa hasira zako unazozijua kwa bahati mbaya unapata ujauzito na bahati mbaya mmeo anagundua kuwa huenda una ujauzito na anajifanya kupotezea

Unaomba ushauri kwa mashost ,wanakushauri fanya kila linalowezekana umpe mmeo tendo kisha utamwambia ujauzito ni wako

Kwa kuwa mwanaume alishagundua kila kitu anakataa na unaanzisha ugomvi kuwa mmeo anakunyima tendo la ndoa

Unaamua kwenda dawati kushtaki, mwanaume anaweka msimamo kuwa kwa sasa hana hisia,anatatizo la nguvu za kiume,mkeo akusubiria kwa wakati huo yupo kwenye matibabu

Hatimaye ujauzito unakuwa mkubwa mwanaume anaamua kuhoji kulikoni? Mwanamke anajitetea kuwa wew mwanaume ndiyo chanzo aliamua kulipa kisasi baada ya kumcheat

Mwanaume anaamua kuwambia ndugu zake na ndugu wa mwanamke,ushauri unatoka kuwa amsamehe walee watoto, mwanaume na huyo mwanamke wamezaa watoto wawili

Jamaa anaamua kuchukua watoto wake anawapeleka shule ya bweni wanabaki wawili nyumbani

Jamaa anaamua kususa kutoa matumizi na ujauzito tarehe zinakaribia za kujifungua,mwanamke hana namna anaona acha avumilie ajifungue mtoto kwa sababu hana sehemu ya kwenda

Kwa bahati mbaya mwanamke anapata shida ya uzazi anaanza bleeding anampigia mwanaume simu na kumwambia aje ampeleke hospital jamaa anakata simu

Mwanamke anajiongeza anamuita jirani,na jirani anatafuta usafiri na kumpeleka hospital ila kwa bahati mbaya anafanyiwa operation na kwa bahati mbaya mtoto alishafariki dunia

Mwanaume anaambiwa gharama za matibabu anasema hahusiki,ndugu na jamaa wanachangisha wanapata hela inayotakiwa wanalipa bill anaruhusiwa kutoka hospital na anaamua kwenda kwao kwa wazazi

Mwanamke anapata ushauri wa kumkamata kwa kumtishia kumuua kwamba hata kile kitoto kufia tumboni ni kipigo cha mwanaume, mwanaume anakamatwa na polisi analala lock up siku ya kwanza anadhaminiwa anatoka baadae polisi wanafuta kesi kwa sababu ushahidi hautoshi kumpeleka mahakamani

Mwanamke anaomba talaka na jamaa anakubali,wakati shauri la talaka linaendelea ghafla mwanamke anakataa shauri la talaka lisiendelee
Anaamua kuita ndugu wa mwanaume na wa kwao anaomba mwanaume msamaha anaomba arudi kwenye ndoa yake yeye process za talaka ameziacha labda mwanaume afungua shauri la talaka,anataka alee watoto wake

Nini kifanyike hapa?
Sio poa jamaa alivyomtia stress mama kijacho hadi mtoto asie na hatia akafa. Angemuhudumia tu kisha baada ya mke kujifungua angemalizana nae kistaarabu.Mbona na Yeye alichepuka au kwa kuwa wanaume hatushiki mimba.Cha kufanya hapo ni kusameheana Kwa kuwa wote wana nakosa ila chanzo ni huyo jamaa.
 

Attachments

  • IMG_20250623_184537.jpg
    IMG_20250623_184537.jpg
    88.2 KB · Views: 4
Back
Top Bottom