Hapa ndipo anapokosea Mkuu wa Mkoa wa Dar

Huna unalolijua mbumbumbu wewe. Jinai huendeshwa na Serikali tu. Uwe unaelewa
Ili serikali ifanye ivo nini kinatakiwa kifanyike? leteni maelekezo ya kutosha basi maana tumechoka na hizi hadithi tujue moja anasepa ama laa.
 
Huyo jamaa ni kichaa, ukishinda unamjadili utapoteza muda bure, ni zaidi ya mwehu huyo
 
Kuna makosa ambayo anayafanya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu tuhuma zinazomkabili. Hadi sasa, mkuu huyo wa mkoa wa Dar anatuhuma mbili zinazoenea: ya kwanza ni ile ya kutumia cheti cha kidato cha nne cha mtu mwingine. Ya pili ni ile ya kuvamia, akiwa na askari wenye silaha, ofisi za Clouds Media.

mKUU UMESAHAHU ILE YA UTAPELI NA KUPORA MALI ZA WATUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA!
 
Umewaza kama mm mkuu,,kama Ruge alisema hawawez kurusha habari ambayo haipo balanced,sasa hawa wamesema hapokei simu,alitokea mlango wa nyumba,lakin habar na hukumu wameitoa sasa waliibalance habar kwa nani?? Na ndio maana zitto akawaambia kwa nn mmetoa hukumu kabla kamati haijaleta majibu?? Maana jukwaa la wahariri wamemuhukumu tayar tena kabla nape hajatoa ripot ya tume iliyoundwa,je usahihi upo wap?
Waandishi wa habari wanaendeshwa na mitandao!.....
 
Haki ya mtu haipotei. Kama mh makonda anasingiziwa, ipo siku ukweli utamweka huru, na kama la, yasemwayo na kuandikwa dhidi yake ni ya kweli, ipo siku ataingia kwenye mikono salama ya polisi. Nayo ndio siku ya kifo cha nyani. kwani husemwa ' u can fool all the people some times, u can fool some people all the times. But u cant fool all the people all the times'. Na hiyo siku si nyingine zaidi ya ile mwandishi mmoja wa vitabu alio iita ' the day the cookies crumbles'.
 
Kuna makosa ambayo anayafanya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu tuhuma zinazomkabili. Hadi sasa, mkuu huyo wa mkoa wa Dar anatuhuma mbili zinazoenea: ya kwanza ni ile ya kutumia cheti cha kidato cha nne cha mtu mwingine. Ya pili ni ile ya kuvamia, akiwa na askari wenye silaha, ofisi za Clouds Media.

Katika hali ya kawaida, tena kwa wanasiasa kama alivyo yeye mkuu wa mkoa wa Dar, tuhuma hujibiwa. Hujibiwa kwa kukanushwa au kukubaliwa kwa kuomba msamaha au kueleza ukweli wa upande wa yule anayetuhumiwa ili kuzionyesha kuwa tuhuma hizo si za kweli na zinapaswa kushindwa. Kuhusu cheti, anapaswa tu kuonyesha cheti chake. Basi.

Kuhusu kuvamia Clouds, anapaswa kujitokeza na kueleza upande wake wa taarifa. Kimsingi, nimesikitishwa na kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dar cha kukwepa kuhojiwa na Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuchunguza uvamizi wa Clouds Media. Kwa mujibu wa Kamati hiyo, mkuu wa mkoa wa Dar 'aliwakimbia' wanakamati waliotaka kumhoji kuhusu kadhia hiyo.

Kujificha katika vita ya madawa ya kulevya hakutamsaidia chochote mkuu wa mkoa wa Dar. Tena, kusifiwa na Rais na kutakiwa kuchapa kazi hakutamsafisha mkuu wa mkoa wa Dar kutoka katika kashfa hizo ambazo zitabaki kama zilivyo na kuendelea kusambaa na kuaminika. Niliwahi kumshauri humu kuwa, kama anachafuliwa akawashtaki wanaomchafua.

Watanzania tulio wengi tunaunga mkono mapambano ya vita ya madawa ya kulevya kwa kuzingatia madhara yake kwa jamii yetu. Tunaunga mkono pia juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi na kustawisha nchi yetu. Lakini, hatuungi mkono kiongozi kuandamwa na tuhuma nzito kama za mkuu wa mkoa wa Dar. Anapaswa kuzitolea ufafanuzi au kuwajibika/kuwajibishwa.

Kusingizia kuwa kila anayekosoa utendaji au maadili ya kiongozi fulani ni mpinzani wa vita ya madawa ya kulevya na utendaji wa Serikali si njia salama ya kumaliza tuhuma za mkuu wa mkoa wa Dar. Tuhuma hujibiwa na ukweli kutoka kwa anayetuhumiwa na si vinginevyo. Watanzania wanapenda maendeleo na utawala wa kisheria.

Mambo yote yanaanza kichwani. Huyu ni Bashite aliyezungusha zero Form 4. Yaani ni kichwa wazi, jinga, halina akili. Ni toto tundu la misheni town. Ni mpiga kabali kwa wazee mf. Waziri Mkuu mstaafu na mfunga kamba za viatu vya wenye pesa mf. riz one. Ukuu wa mkoa ni maji marefu kwake. Ni bongo lala huyu Daudi Bashite. Ni aibu kutawaliwa na Bashite karne ya 21 mkoa wenye vyuo vikuu kibao!!!
 
Kaka Pascal Mayalla, who is insane? Chunga sana na lugha yako isiyo ya staha. Eleza bila kukwaza hata kwa matumizi ya lugha, utaeleweka tu.
Kimsingi, nimesikitishwa na kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dar cha kukwepa kuhojiwa na Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuchunguza uvamizi wa Clouds Media. Kwa mujibu wa Kamati hiyo, mkuu wa mkoa wa Dar 'aliwakimbia' wanakamati waliotaka kumhoji kuhusu kadhia hiyo.
Mkuu
Petro E. Mselewa
Mtu mwenye akili zake timamu anaweza kufanya jambo la kitoto na kijinga kama hili?. Tukisema jamaa ni insane, tunalaumiwa kutumia lugha ya machukizo, hebu basi nitafutie neno tamu na la kupendeze kuielezea tabia hii.

Paskali
 
Kuna makosa ambayo anayafanya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu tuhuma zinazomkabili. Hadi sasa, mkuu huyo wa mkoa wa Dar anatuhuma mbili zinazoenea: ya kwanza ni ile ya kutumia cheti cha kidato cha nne cha mtu mwingine. Ya pili ni ile ya kuvamia, akiwa na askari wenye silaha, ofisi za Clouds Media.

Katika hali ya kawaida, tena kwa wanasiasa kama alivyo yeye mkuu wa mkoa wa Dar, tuhuma hujibiwa. Hujibiwa kwa kukanushwa au kukubaliwa kwa kuomba msamaha au kueleza ukweli wa upande wa yule anayetuhumiwa ili kuzionyesha kuwa tuhuma hizo si za kweli na zinapaswa kushindwa. Kuhusu cheti, anapaswa tu kuonyesha cheti chake. Basi.

Kuhusu kuvamia Clouds, anapaswa kujitokeza na kueleza upande wake wa taarifa. Kimsingi, nimesikitishwa na kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dar cha kukwepa kuhojiwa na Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuchunguza uvamizi wa Clouds Media. Kwa mujibu wa Kamati hiyo, mkuu wa mkoa wa Dar 'aliwakimbia' wanakamati waliotaka kumhoji kuhusu kadhia hiyo.

Kujificha katika vita ya madawa ya kulevya hakutamsaidia chochote mkuu wa mkoa wa Dar. Tena, kusifiwa na Rais na kutakiwa kuchapa kazi hakutamsafisha mkuu wa mkoa wa Dar kutoka katika kashfa hizo ambazo zitabaki kama zilivyo na kuendelea kusambaa na kuaminika. Niliwahi kumshauri humu kuwa, kama anachafuliwa akawashtaki wanaomchafua.

Watanzania tulio wengi tunaunga mkono mapambano ya vita ya madawa ya kulevya kwa kuzingatia madhara yake kwa jamii yetu. Tunaunga mkono pia juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi na kustawisha nchi yetu. Lakini, hatuungi mkono kiongozi kuandamwa na tuhuma nzito kama za mkuu wa mkoa wa Dar. Anapaswa kuzitolea ufafanuzi au kuwajibika/kuwajibishwa.

Kusingizia kuwa kila anayekosoa utendaji au maadili ya kiongozi fulani ni mpinzani wa vita ya madawa ya kulevya na utendaji wa Serikali si njia salama ya kumaliza tuhuma za mkuu wa mkoa wa Dar. Tuhuma hujibiwa na ukweli kutoka kwa anayetuhumiwa na si vinginevyo. Watanzania wanapenda maendeleo na utawala wa kisheria.
Alipokuwa anataja mlisema anakimbiza watuhumiwa, juzi kaenda kimyakimya mnasema kavamia!!khaa waswahili bhana
 
Kwahiyo alikwenda Clouds Media kuwasaka watuhumiwa wa madawa ya kulevya? Bure kabisa wewe!
 
Haki ya mtu haipotei. Kama mh makonda anasingiziwa, ipo siku ukweli utamweka huru, na kama la, yasemwayo na kuandikwa dhidi yake ni ya kweli, ipo siku ataingia kwenye mikono salama ya polisi. Nayo ndio siku ya kifo cha nyani. kwani husemwa ' u can fool all the people some times, u can fool some people all the times. But u cant fool all the people all the times'. Na hiyo siku si nyingine zaidi ya ile mwandishi mmoja wa vitabu alio iita ' the day the cookies crumbles'.
Yeye ndiye wa kumaliza suala lake. Who else?
 
Paul Makonda ana matatizo ya kisaikolojia. Huwezi fanya haya mambo yote ukiwa na akili timamu kabisa.
Hana busara wala hekima hii unaona kupitia matendo yake.

Mkuu wa mkoa hana na hajui maadili ya uongozi. Hajui maana ya accountability, responsibility na umuhimu wa morals kwa kiongozi.

Kutiliwa shaka ya kughushi cheti ni doa kubea sana kwa kiongozi wa umma. Alitakiwa approve wrong wanaomtuhumu au achie ngazi kama kweli kaghushi. Kama wengi mnavyojua mfano wa Waziri mmoja huko Ujerumani alivyolazimika kujiuzulu kwa kkosa na unakili katika masomo yakr ya uzamivu.

Kwa sababu gani alijiuzulu? Asingekuea na mamlaka ya kimaadili kukemea au kumchukulia hatua mtumishi aliyeyuhumiwa kwa kosa kama lake...au kosa lingine lolote kwa sababu na yeye ni mkosa... makosa yake yalichukuliwa poa na hivyo nae inabidi achukulie poa makosa ya wengine.
 
Makonda , bashite
Nilifikiri itakuja *********** kumbe yasharuhusiwa. Basi powa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom