Hapa ndipo anapokosea Mkuu wa Mkoa wa Dar

Hapa ndipo anapokosea Mkuu wa Mkoa wa Dar

Unaujua utaratibu wa kufungua mashtaka ya jinai au unaongea tuu? Kesi ya jinai sio kama kesi ya talaka mkuu! Jinai ni ya Jamhuri na inashughulikiwa na ofisi ya DPP.


Kwa hiyo Meya wa chadema alidanganya Umma alivyosema atamshitaki Mkuu wa Mkoa?
 
si bure kuna anaenpa kiburi. Kama hana basi anavitu anavyojivunia
IMG_20170322_072438.JPG
 
Mselewa:Hivi wale askari alioongozana nao usiku walipata ruhusa toka kwa nani? Maana kwa taratibu za kijeshi na kipolisi unapochukua silaha ghalani lazima ijulikane unaipeleka wapi na lazima usaini. Huyo aliyewasainisha maaskari wa Makonda aliambiwa silaha zinaenda kufanya nini usiku? Ujambazi uananzaga hivihivi na hawa askari wetu huwakodishia majambazi silaha hivihivi.
 
Kuna makosa ambayo anayafanya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu tuhuma zinazomkabili. Hadi sasa, mkuu huyo wa mkoa wa Dar anatuhuma mbili zinazoenea: ya kwanza ni ile ya kutumia cheti cha kidato cha nne cha mtu mwingine. Ya pili ni ile ya kuvamia, akiwa na askari wenye silaha, ofisi za Clouds Media.

Katika hali ya kawaida, tena kwa wanasiasa kama alivyo yeye mkuu wa mkoa wa Dar, tuhuma hujibiwa. Hujibiwa kwa kukanushwa au kukubaliwa kwa kuomba msamaha au kueleza ukweli wa upande wa yule anayetuhumiwa ili kuzionyesha kuwa tuhuma hizo si za kweli na zinapaswa kushindwa. Kuhusu cheti, anapaswa tu kuonyesha cheti chake. Basi.

Kuhusu kuvamia Clouds, anapaswa kujitokeza na kueleza upande wake wa taarifa. Kimsingi, nimesikitishwa na kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dar cha kukwepa kuhojiwa na Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuchunguza uvamizi wa Clouds Media. Kwa mujibu wa Kamati hiyo, mkuu wa mkoa wa Dar 'aliwakimbia' wanakamati waliotaka kumhoji kuhusu kadhia hiyo.

Kujificha katika vita ya madawa ya kulevya hakutamsaidia chochote mkuu wa mkoa wa Dar. Tena, kusifiwa na Rais na kutakiwa kuchapa kazi hakutamsafisha mkuu wa mkoa wa Dar kutoka katika kashfa hizo ambazo zitabaki kama zilivyo na kuendelea kusambaa na kuaminika. Niliwahi kumshauri humu kuwa, kama anachafuliwa akawashtaki wanaomchafua.

Watanzania tulio wengi tunaunga mkono mapambano ya vita ya madawa ya kulevya kwa kuzingatia madhara yake kwa jamii yetu. Tunaunga mkono pia juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi na kustawisha nchi yetu. Lakini, hatuungi mkono kiongozi kuandamwa na tuhuma nzito kama za mkuu wa mkoa wa Dar. Anapaswa kuzitolea ufafanuzi au kuwajibika/kuwajibishwa.

Kusingizia kuwa kila anayekosoa utendaji au maadili ya kiongozi fulani ni mpinzani wa vita ya madawa ya kulevya na utendaji wa Serikali si njia salama ya kumaliza tuhuma za mkuu wa mkoa wa Dar. Tuhuma hujibiwa na ukweli kutoka kwa anayetuhumiwa na si vinginevyo. Watanzania wanapenda maendeleo na utawala wa kisheria.
Umelieleza kifasaha sana ndugu yangu, lakini tatizo letu kubwa hapa JF ni kwamba watu tunakataa ukweli kwa visingizio vya itikadi zetu. Watu kama kina Magufuli na Mkonda wanafanya hivyo sababu kubwa moja watu wanaowaongoza wamejigawa katika makundi kwa maana hawana umoja. Pamoja na maelezo yako mazuri uliyayandika watu watakupinga bila kutoa sababu muhimu zaidi ya mihemuko ya kisiasa.
 
Kwenye Hili Ni Lazima Waziri Mkuu Anyofolewe au Ikiwezekana Ku-impeach Mkuu wa Nchi. JPM Ndiye Aliyemtuma Makonda Kufanya Upuuzi Wote Huu na Kama Hajamtuma Kwanini Hamtoi?

Ni Jukumu la Watu Wote Kuwalilia Wabunge Wetu Wafanye Tunayotaka na Kuwaondoa Kama Si Majaliwa Basi John Pombe Maharage Mwenyewe.

Hawaiwezakani Mawaziri Husika Wote Wako Kimya (Ukitoa Nape), Wanaopiga Kelele ni Wabunge Wasio na Dhamana na Serikali na Wananchi pekee .
 
Kujificha katika vita ya madawa ya kulevya hakutamsaidia chochote mkuu wa mkoa wa Dar.
Wapo maboya ambao hadi leo wanaamini katika huo utumbo lakini ukiwauliza ni drug dealer gani ambae amefikishwa mahakamani hadi sasa; hakuna atakayekupa jibu!!!
 
Vyombo vya habari vimetoa tamko kuwa vitakua havimpi ushirikiano. ......cha kushangaza kamati nayo inalalamika kuwa aliwatoroka....kiufupi hamtaki kumpa ushirikiano....nae hawapi ushirikiano....lkn cha ajabu mnajinasibu kuwa mnafanyakazi kiprofeshiono....lkn mbona taarifa ya kamati haijabalance ...yaani haina upande wapili lakini imetolewa?
Umewaza kama mm mkuu,,kama Ruge alisema hawawez kurusha habari ambayo haipo balanced,sasa hawa wamesema hapokei simu,alitokea mlango wa nyumba,lakin habar na hukumu wameitoa sasa waliibalance habar kwa nani?? Na ndio maana zitto akawaambia kwa nn mmetoa hukumu kabla kamati haijaleta majibu?? Maana jukwaa la wahariri wamemuhukumu tayar tena kabla nape hajatoa ripot ya tume iliyoundwa,je usahihi upo wap?
 
Mselewa wewe mwanasheria,nikuulize,hivi sheria zetu zinazungumziaje insanity kama kikwazo cha kuteuliwa uongozi?Au ziko kimya?
 
Hawezi kukanusha juu ya kutumia vyeti feki never Bashite ni kilaza aliyebobea ndio maana ukilaza wake waendana na upopoma alioufanya pale clouds kwa mtu mwenye akili timamu aliyesoma chuo hawezi kufanya ujinga ule
 
Viongozi wetu Africa waroho wa Madaraka Mtu kama Makonda Nchi za wenzetu angekua ashapiga chini ukuu wa mkoa anasubiri Uchunguzi na hili suala la Makonda tunaweza kuwalaumu Wakoloni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom