Hapa ndipo anapokosea Mkuu wa Mkoa wa Dar

Hapa ndipo anapokosea Mkuu wa Mkoa wa Dar

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,350
Reaction score
26,166
Kuna makosa ambayo anayafanya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu tuhuma zinazomkabili. Hadi sasa, mkuu huyo wa mkoa wa Dar anatuhuma mbili zinazoenea: ya kwanza ni ile ya kutumia cheti cha kidato cha nne cha mtu mwingine. Ya pili ni ile ya kuvamia, akiwa na askari wenye silaha, ofisi za Clouds Media.

Katika hali ya kawaida, tena kwa wanasiasa kama alivyo yeye mkuu wa mkoa wa Dar, tuhuma hujibiwa. Hujibiwa kwa kukanushwa au kukubaliwa kwa kuomba msamaha au kueleza ukweli wa upande wa yule anayetuhumiwa ili kuzionyesha kuwa tuhuma hizo si za kweli na zinapaswa kushindwa. Kuhusu cheti, anapaswa tu kuonyesha cheti chake. Basi.

Kuhusu kuvamia Clouds, anapaswa kujitokeza na kueleza upande wake wa taarifa. Kimsingi, nimesikitishwa na kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dar cha kukwepa kuhojiwa na Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuchunguza uvamizi wa Clouds Media. Kwa mujibu wa Kamati hiyo, mkuu wa mkoa wa Dar 'aliwakimbia' wanakamati waliotaka kumhoji kuhusu kadhia hiyo.

Kujificha katika vita ya madawa ya kulevya hakutamsaidia chochote mkuu wa mkoa wa Dar. Tena, kusifiwa na Rais na kutakiwa kuchapa kazi hakutamsafisha mkuu wa mkoa wa Dar kutoka katika kashfa hizo ambazo zitabaki kama zilivyo na kuendelea kusambaa na kuaminika. Niliwahi kumshauri humu kuwa, kama anachafuliwa akawashtaki wanaomchafua.

Watanzania tulio wengi tunaunga mkono mapambano ya vita ya madawa ya kulevya kwa kuzingatia madhara yake kwa jamii yetu. Tunaunga mkono pia juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi na kustawisha nchi yetu. Lakini, hatuungi mkono kiongozi kuandamwa na tuhuma nzito kama za mkuu wa mkoa wa Dar. Anapaswa kuzitolea ufafanuzi au kuwajibika/kuwajibishwa.

Kusingizia kuwa kila anayekosoa utendaji au maadili ya kiongozi fulani ni mpinzani wa vita ya madawa ya kulevya na utendaji wa Serikali si njia salama ya kumaliza tuhuma za mkuu wa mkoa wa Dar. Tuhuma hujibiwa na ukweli kutoka kwa anayetuhumiwa na si vinginevyo. Watanzania wanapenda maendeleo na utawala wa kisheria.
 
tuhuma zinazomkabili anatakiwa awe jela nashangaa bado anaendelea kutuibia kwa kufanya forgery kwa sababu akili hana hata kidogo anajiwekea mgongo wa madawa !!kosa halirekebishwi kwa kufanya kosa labda sheria za mfalme ambae mzizi wake ameuchimbia chini

mahakama zetu zinafanya nini?kwanini wasiweke injuction Bashite asiendelee kutuibia na kuhujumu uchumi?
 
tuhuma zinazomkabili anatakiwa awe jela nashangaa bado anaendelea kutuibia kwa kufanya forgery kwa sababu akili hana hata kidogo anajiwekea mgongo wa madawa !!kosa halirekebishwi kwa kufanya kosa labda sheria za mfalme ambae mzizi wake ameuchimbia chini

mahakama zetu zinafanya nini?kwanini wasiweke injuction Bashite asiendelee kutuibia na kuhujumu uchumi?
Mkuu wanaostahili kuchukua hatua hizi ni IGP DPP na idara zao za "Inteligensia" ambao kila kukicha wapo mitandaoni

Sent from my Vodafone 875 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom