Hapa ndio ninapotofautiana na Kibonde

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Jumatatu katika kipindi cha Jahazi bwana kibonde alisema, tofauti na huku kwetu kule marekani hata mtu awe mjinga vipi anaweza tu kuongoza ile nchi, alisema mfumo wa marekani unawezesha mtu yeyote kuwa rais na akaongoza nchi vizuri tu, niliposikia hii nilishangaa, lakini leo wakati nasikiliza debate ya Obama vs Romney nikakumbuka zile kauli za bwana kibonde, nikatamani kama awe anatazama pia ili atafakari.

Wakati wanasiasa wetu wanafanya siasa 'uchwara' wenzetu wako detailed sana, kwa mfano, kutakuwa na debate tatu mwaka huu, zote kwa dk 90 na zote zinarushwa live.

debate ya kwanza ilikua kuhusu domestic policy, ya pili kuhusu domestic na foreign policy na ya tatu itakuwa foreign policy, na kwa debate zote hizi kuna scrutiny kubwa sana kutoka media na kutoka wananchi.

ni kama job interview, kama hujui hupiti unless kuna rushwa, ambayo kwa bahai nzuri tena kwa wenzetu haina nafasi kabisa
!
 
Wameharibu sana kipindi cha Jahazi kinapumulia O2, wanajikuta wenyewe wanabisha mambo ya kipuuzi sana ambayo hayana tija kwa taifa.
 
mjinga atawezaje kuongoza taifa kubwa kama hilo,kila dakika wanawaza wapi wataiba mafuta,gesi,madini na kwenda sayari nyingine kuangalia kama nako kuna mafuta,gesi,madini na maliasili nyingine na jinsi gani watazileta duniani,ni taifa lenye changamoto kubwa sana.
 
Jumatatu katika kipindi cha Jahazi bwana kibonde alisema, tofauti na huku kwetu kule marekani hata mtu awe mjinga vipi anaweza tu kuongoza ile nchi, alisema mfumo wa marekani unawezesha mtu yeyote kuwa rais na akaongoza nchi vizuri tu, niliposikia hii nilishangaa, lakini leo wakati nasikiliza debate ya Obama vs Romney nikakumbuka zile kauli za bwana kibonde, nikatamani kama awe anatazama pia ili atafakari.

Wakati wanasiasa wetu wanafanya siasa 'uchwara' wenzetu wako detailed sana, kwa mfano, kutakuwa na debate tatu mwaka huu, zote kwa dk 90 na zote zinarushwa live.

debate ya kwanza ilikua kuhusu domestic policy, ya pili kuhusu domestic na foreign policy na ya tatu itakuwa foreign policy, na kwa debate zote hizi kuna scrutiny kubwa sana kutoka media na kutoka wananchi.

ni kama job interview, kama hujui hupiti unless kuna rushwa!

Ndugu yangu mtu pekee asiyetofautiana na Kibonde ni Joseph Kusaga..........wengine wote twatofautiana naye........hata mkwewe pia
 
Akili za huyo jamaa ni sawa na jina lake
Anadhani kwa vile amejaliwa sauti na maneno mengi, na akili pia anayo kumbe empty brain..
Anadhani kwa vile marekani imeendelea, basi hakuna tena changamoto. Thatz a very poor conceptualization.. Haelewi kama marekani ndio wenye changamoto nyingi na nzito kuliko..
Poor ki***nde!!!
 
"Kauli za Kibonde, kipimo cha uelewa wake". Kibonde ni mtangazaji "presenter". Hili kundi halina uelewa wa mambo sana kwa sababu wanapresent chochote wanachokijua. Kwake yeye alichosema ndicho anachokifaham! Mi sipati shida wala siwezi kubishana nae kwa sababu hana utetezi wa anachobishania (he is not rationalist). Mwacheni hakuna haja ya kumbadilisha.
 
huyo ni "KIBONDE" kweli
chezea kibonde wewe
kajamaa kanaboa sana coz kila kitu kanajifanya kanajua
while hopeless kabisa
 
Jamani hebu nisaidieni kwanza kujua kiwango cha elimu cha huyo Bwana Kibonde ndio niendelee kutoa mchango wangu kwani vitu anavyoongea sidhani kama anao ufahamu wa kutosha.
 
unahangaika na watu wenye kudhani wanafikiri sana kumbe mengi wanyoongea wanaudanganya umma!kuna kitu namkubali kibonde "anajua mizaha na maskhara" ndio kitu kianchonifanya nisikilize jahazi lakini sio upeo,uelewa na uchambuzi wa mambo muhimu ya nchi na ya kimataifa!
 
mi nafikiri alishindwa kufafanua kauli yake tofauti yetu na Marekani katiba ya Marekani inambana rais kufanya maamuzi kinyume na katiba kwa maana akivunja mtu yeyote ana haki ya kumshitaki kwa hiyo haijarishi mmechagua rais wa namna gani lazima aongoze kwa kufata katiba lakini huku kwetu tumempa rais madaraka makubwa kwa lugha nyingine rais yuko juu ya katiba hata akiivunja hatuwezi kumfanya lolote ndio maana hayati Mw.Nyerere alisema kwa katiba hii angeweza kuwa juu ya sheria.
Kwa lugha rais katiba ya marekani ina kinga wakati ya kwetu haina kinga simpendi Kibonde ila ukweli ndio huu hata uchague rais mjinga marekani lakienda kinyume cha katiba imekula kwake
 
Kibonde is right. America wana Institution siye tuna mtu, thats why Zidumu Fikra za Mwenyekiti mpaka leo Zinafanya kazi. i.e Zamu ya wamama... sasa.

ukiwa mbovu huwezi kufika white house, jamaa wako makini sana!
 
Back
Top Bottom