Superboy
Member
- Sep 17, 2013
- 45
- 6
Kuna mdada wa senegal alikimbia vita liberia yupo senegal kwenye camp ya wakimbizi sasa kuna pesa ziliachwa na wazazi wake bank ya scotland na kwenye urithi aliandikwa yeye. Siku akatuma maombi ya kuzitaka hizo pesa bank wakamwambia atafute mtanzania ili pesa zi hamishiwe kwa huyo mtanzania. Halafu atafute mwanasheria aliye sajiliwa wa senegal akaingia fb akaniona akanitumia email tukawasiliana fresh akanipa anwani za hiyo bank nilipowasiliana nao wakasema nitafute hati ya kiapo kwa mwanasheria wa senegal nikamwambia yule mdada akaniunganisha na huyo mwanasheria sasa anataka$700 ili aniandikie ampe huyo mdada asaini hiyo hati yenye details zangu ikiwemo akaunt yangu ya bank na apeleke kule bank na benk wanasema wakiipata tu hiyo hati na vyeti vya kifo cha huyo baba yake mdada wananitumia hiyo hela hapohapo halafu yule mdada aje aichukulie kwangu na kuna asilimia ananiachia. Kila kitu kimekamilika bado hiyo hati tu na kuipata inatakiwa nimtumie mwanasheria $700. Kinachonitia wasiwasi mbona kila kukicha wanaoniomba niwasaidie inshu kama hii wanaongezeka kila kukicha.